KILIMANJARO katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi za taifa, wizara ya maliasili na
utalii imeanza mkakati wa kuanzisha mfuko maalumu wahifadhi wa mazingira, ambao
ni endelevu kwaajili huifadhi wa mlima
Kilimanjaro na mlima meru utakaotumika
na jamii inayozunguka milima hiyo kwa
kuwapatia elimu ya kulinda mfumo wa
kiikolojia pia kuwawezesha kiuchumi.
Waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu, alisema hayo mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro, kwenye kikao kilicho washirikisha baadhi ya wabunge
na watendaji wa serikali, ambapo alisema mfuko huo ni maombi ya
wabunge wa mkoa huo, na utatekelezwa
na wizaza ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na wadau wa mazingira.
Alisema kila mwaka Tanzania
inapoteza wastani wa hekta 375,000 za
miti, na kwamba baada ya miaka 15 nchi inaweza kugeuka jangwa, hiyo niwajibu wa serikali kutafuta suluhisho
kwa kukomboa mfumo wa kiikolojia , mfumo wa miti ,mfumo wa maisha na mfumo wa mito
ambayo inatiririsha maji kutoka tao la milima
ya Kilimanjaro na Meru.
Naibu waziri tawala za mikoa na serikali za mitaa, ambaye
pia ni mbunge wa Wilaya ya siha Aggrey Mwanri, amesema baada ya kuonauharibifu
wa mazingira ikiendelea kwakasi karika hifadhi ya mlima kilimanjaro ,wabunge wa
mkoa huo walipeleka kilio hicho serikalini ili kukpataufumbuzi wa tatizo hilo, ambalo
lingeweza kuifanya nchi kugeuka jangwa.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya ardhi maliasili na
mazingira Abdulkarim Shah, alisema ili
mpango wa kuhifadhi mazingira uweze kuwa
endelevu ni muhimu kupeleka elimu ya
utunzaji mazingira kwa kuanzia katika shule za msingi ili wanafunzi waweze kutambua umuhimu wa
kuyatunza mazingira.
No comments:
Post a Comment