Wafanyabiashara wa Mkoa wa kilimanjaro wamejitokeza kumuunga mkono Mfanyabiashara anayemiliki kampuni ya Mafuta ya Magari na Kampuni ya Vifaa vya Magari Ya Ngiloi Ulomi Enterprisess na Panone and Co. ltd katika kuisaidia Timu ya Mpira wa Miguu ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Panone Football Club inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza.
Mmiliki wa Kampuni ya Ibra Line ndugu Ibrahim Shayo akizungumza na Mwandishi wetu ofisini kwake.
Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti na mwanahabari wa King Jofa walitoa Rai juu ya Nia yao ya dhati ya kuisaidia timu ya Panone Fc baada ya kuona kuwa ina malengo makubwa na Kugundua kuwa si timu ya Mtu binafsi bali ni timu yao. Mmoja wa wafanyabiashara hao Ndugu Ibahim Shayo mmiliki wa kampuni ya Usafirishaji ya Ibra Line alisema ni vema wananchi wa kilimanjaro wakajivunia na cha kwao kuliko kujivunia na vya watu na huu ni wakati muafaka wa kuweza kujitoa kuisaidia PAnone Football Club iweze kushiriki Ligi Kuu Tanzania bara badala ya kusubiri kuona timu za wenzetu tu.
Nae mmiliki wa kampuni ya LRM Investment ndugu Didas Mushi kwa upande wake alisema hapo awali alijua Timu ya Panone Fc ni timu ya Kampuni ya Panone and Co. Ltd lakini baada ya kugundua kuwa Mmiliki wa Panone and Co. Ltd alikua akiisaidia timu hiyo ya vijana toka ikiwa chini ndipo wakaamua kuiita jina la Panone. Ndipo alipoona ni vyema akagawa sehemu ya Faida yake katika kuisaidia timu hiyo ya vijana wa Kilimanjaro ya Panone Fc.
Panone Fc ni timu ya mkoa wa Kilimanjaro inayoundwa na VIjana wa Mkoa wa kilimanjaro wenye hari na Malengo ya Kuirudisha Ligi kuu katika Mkoa wa Kilimanjaro baada ya Takribani Miaka ishirini kupita. Timu hii imeweza kushiriki ligi ya mkoa wa kilimanjaro na kupata tiketi ya Kuuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro katika MAshindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa ambapo Timu hiyo ilipangiwa katika kituo cha Mbeya na Kuibuka na UShindi. Kutokana na ushindi huo ndipo walipopanda Daraja na kupata tiketi ya kushiriki Ligi Daraja la kwanza. Katika kipindi chote hicho Timu ya Panone Fc ilikua ikihudumiwa na Mr. Patrick Ngiloi kupitia kampuni yake ya Panone and co. ltd mpaka sasa Waafanyabiashara hao walipoona ni wakati wa kumuunga mkono. Wafanyabiashara waliojitokeza kuiunga mkono timu hiyo mpaka sasa ni Didas Mushi (LRM INVESTMENT), Ment Mbowe (Machame Safari), Richard Munuo, Karia, Ibrahim Shayo (IBRA LINE), Mr. Cuthbert (AHSANTE TOURS).
TUJIKUMBUSHE:
Ikumbukwe Timu ya Panone Fc inahitaji kufanya vyema katika mashindano ya Ligi Daraja la kwanza ili iweze kupata nafasi ya kushiriki Ligi kuu na huu ni wasaa wa Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kilimanjaro na Walio nje ya Mkoa wa Kilimanjaro kuiunga mkono timu ya Panone Fc ili iweze kuleta heshima ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro unaoaminika kuwa hauna uwezo wa kisoka tena baada ya Timu ya Ushirika.
No comments:
Post a Comment