KILIMANJARO hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Naomi Mwerinde, amemhukumu Evarist Arobogast (24) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na kosa la kumlawiti mtoto wa miaka saba na kumuumiza vibaya sehamu za siri.
Hakimu mwerinde alisema
mshtakiwa huyo mkazi wa kijiji cha kirongo juu wilayani Rombo atatumikia kifungo
cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba.
Mwendesha
mashtaka wa Polisi, Raymond Sikukuu aliieleza mahakama kuwa mshtakiwa
alimvamia na kumlawiti mtoto huyo wa miaka saba na kumuumiza vibaya
sehemu za siri.
Sikukuu alidai kuwa mnamo tarehe 24 machi mwaka huu katika kijiji cha kirongo juu Usseri ambapo mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na kumsababishiwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Mwendesha
mashtaka huyo alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria ya 154 sura 16 ya kanuni ya sheria ya adhabu iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Mwerinde alisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka hilo pasipo kuacha shaka.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Mwerinde alisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka hilo pasipo kuacha shaka.
Hakimu
huyo alisema pia maelezo ya daktari yaliyowasilishwa mahamani hapa
imeonesha kuwa mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili.
Hakimu Mwerinde alisema kuwa vitendo vya ubakaji na ulawiti katika wilaya ya Rombo vimeshamiri kwani katika mahakama hiyo zipo kesi nyingi za kulawiti.
Hakimu Mwerinde alisema kuwa vitendo vya ubakaji na ulawiti katika wilaya ya Rombo vimeshamiri kwani katika mahakama hiyo zipo kesi nyingi za kulawiti.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo mshtakiwa atatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwake na kwa watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo hiyo kwa watoto wadogo.
No comments:
Post a Comment