KILIMANJARO watu
16
ambao ni wakazi wa kijiji cha miti mirefu na Sanya Juu Wilayani Siha
Mkoani Kilimanjaro, wamefishikishwa katika mahakama ya wilaya ya Hai kwa
makosa matatu ya kuvamia shamba la Mwekezaji wa kampuni ya Tanganyika
Film and Safari Tawi la Ndarakwai na kuchoma mali mbalimbali
zenye zaidi ya thamani ya shilingi bilioni 1.7
Akisoma
hati ya
mashtaka mahakamani hapo mwendesha mashtaka Roymax Membe, mbele ya
hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Denis Mpelembwa, amesema kuwa
watuhumiwa hao wote kwa pamoja walitenda makosa hayo kwa kuvamia
shamba la Ndarakwai linalomikiwa na mwekezaji Peter Jones mnamo
Novemba 14 mwaka huu.
Alisema
kuwa
watuhumiwa hao walitenda kosa la kwanza la kuingia ndani ya shamba la
Ndarakwai na kuchoma magari 6 ya kambi ya utalii ya Ndarakwai yenye
thamani ya shilingi milioni 450 ambapo ni kinyume na makaosa ya jinai
kifungu cha 299 ya makosa ya jinai ya mwaka 2002.
Amesema watu hao pia walitenda kosa la pili la kuharibu mali kwa
makusudi za mwekezaji huyo, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni
1 ambapo kosa la tatu watuhumiwa hao walichoma mali za mwekezaji huyo
zenye thamani ya shilingi milioni 210 kinyume na kifungu cha 326 (i) ya
makosa ya jinai ya mwaka 2002.
Membe aliwataja watuhumiwa hao ambao wamefikishwa katika mahaka hiyo
kuwa ni Matey Hilita (42), Julias Daudi (45), Elipokea Sefano (42), Andrea
Elias (67), Alex filipo (30), Victor Joakimu (32), Dicksoni Mallya
(38), wote wakazi wa kijiji cha Miti Mirefu.
Wengine waliofikishwa mahamakani ni Dicksoni Kweka (62), Emanueli Isaya
(17), wakazi wa Sanya Juu, Erick Wilsoni (27), Rael Paulo (26), Bibiana
Charles (36), Hellen stepahano (39), Hellen Daudi (26), na Monika Rongai (42)
wote wakazi wa kijiji cha Miti Mirefu.
Hata hivyo mwendesha mashtaka huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa
upelelezi wa kesi hiyo haujakalika na kuiomba mahakama kutowapa dhamana
watuhumiwa hao kutokana na thamanani halisi ya vitu vilivyoharibu bado
haijajulikana.
Hata hivyo watumuhiwa wote wamekana mashtaka hayo, na hakimu
Mpelembwa alikubali ombi la mwendesha mashtaka huyo na kutoa siku saba
awakilishe thamani halisi ya uharibifu huo na kesi imeairishwa hadi
tarehe 2 Desemba mwaka huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment