KILIMANJARO serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi imeombwa kuchunguza uongozi wa chuo cha polisi
Moshi ili kuondoa migogoro ya baadhi askari wenye ulemavu na magonjwa ya kudumu
walipelekwa chuoni hapo kusoma na kupanda vyeo.
Hatua hiyo imekuja baada ya askari 84 waliofukuzwa na uongozi
wa chuo hicho kwaajili ya kushindwa
kufanya mazoezi ya kijeshi kutokana na kuwa na magonjwa ya kudumu ikiwa ni
pamoja na ulemavu waliopata wakiwa kazini kuendelea kuzuiwa kufanya mtihani wa
mwisho licha ya agizo kutoka makao makuu ya jeshi hilo kutakiwa kurudishwa
chuoni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakifanya mahojiano
na waandishi wa habari, baadhi ya askari hao ambao hawakutaka majina yao
yaandikwe gazetini walisema wizara ya mambo ya ndani nchi ni
vema ikafanya uchunguzi ili kubaini matatizo yaliopo chuoni hapo.
Walisema uchunguzi huo
utasaidia kuondoa migogoro ya upandaji wa vyeo kwa askari wenye ulemavu na
magonjwa ya kudumu kwani uvunjifu wa haki za binadamu umekuwa ukifanywa na
uongozi wa chuo hicho pasipo kujali wagonjwa.
Aidha walisema wamekuwa wakisoma masomo hayo ili kupanda vyeo
na mishahara yao izidi kuboreshwa ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayo
wakabili askari na kwamba serikali ni vema ikaangali sula hilo kwa maslahi ya
askari wote.
Akijubu malalamiko hayo ya askari hao kuzuiwa kufanya
mitihani hiyo Mkuu wa chuo hicho Matanga Mbushi alisema yeye hausiki na
kurudishwa chuo kwa askari na kwamba suala la kufanya mitihani makao makuu ndio watatoa maelekezo
zaidi.
No comments:
Post a Comment