KILIAMANJARO upungufu wa
maji katika Manispaa ya Moshi linaekea kuwa historia ifikapo mwezi Desemba
mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya
Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 382.
Akizungumza
wakati wa ziara ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro, waliotembelea mradi
huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA),
Mhandisi Cyprian Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia
maeneo ya Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.
Mhandisi
Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa
maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa
upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.
Amesema
mradi huo utasaidia kuongeza kiwango cha
upatikanaji wa maji kwa mita za ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa
kusambazia maji ambapo kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia 99.
Amefafanua
kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo
kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo
itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.
Sambamba na
hilo, Mamlaka hiyo imeiomba serikali kuwatumia watalamu wa ndani ya nchi katika
masuala mbambali kwani imefanikiwa kutekeleza mpango wa matokeo makubwa kwa
kutekeleza mradi mkubwa wa maji kwa kutumia wataalam wake wa ndani.
Kwa upande
wake Mhandisi wa mradi huo Said Mrindoko,
amesema zipo changamoto mbalimbali ambazo walikumbana nazo wakati wa
ujenzi wa mradi huo ikiwemo baadhi ya wananchi kujenga karibu na chanzo cha
maji hivyo kusababisha kazi ya kulaza mabomba kuwa ngumu.
Mrindoko amesema
pia wapo baadhi ya wananchi walikataa maeneo yao yasitumike katika ujenzi wa
mradi hali iliyoilazimu mamlaka kuyanunua maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment