KILIMANJARO Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro, kimesema kimejipanga
vizuri katika kuhakikisha kuwa kinarudisha majimbo yote yanayoshikiliwa na
upinzani mkoani humo katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na uchaguzi wa serikali
za mitaa.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha
Tsuduni wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Deogratius
Rutta, alisema chama hicho kimejipanga kikamilifu na kitahakikisha, kinaibuka
na ushindi wa kishindo katika chaguzi hizo.
Katibu huyo alisema pamoja na kuwepo kwa Muungano wa vyama vinne vya upinzani chini ya mwavuli wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA ) wao hawatishiki na kwamba wamejipanga vizuri,kurudisha majimbo yote yanayoshikiliwa na Upinzani kwa sasa mkoani Kilimanjaro.
Ruta alisema muungano wa vyama vya upinzani, hauna tija kwa CCM na serikali, bali muungano huo utaendelea kushuhudia chama hicho kinapata ushindi wa kishindo kwa kupewa ridhaa hiyo na wananchi na kuendelea kuongoza nchi kwa amani na utulivu kama ilivyo kwa hivi sasa.
Adha katika mkutano huo Katibu huyo alipata frusa ya kupokea wanachama wapya wawili kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Tsuduni Exaud Masam kwa tiketi ya Chadema,.
Awali akizungumza
mwenyekiti huyo wa kijiji cha Tsuduni kwa tiketi ya Chadema, Exaud Masamu alisema ameitumikia serikali ya kijiji kwa miaka mitano na kwamba
ameamua kuhama chama hicho kutokana na ukosefu wa ushirikiano kwa baadhi ya
viongozi wa chama hicho.
Aidha
alisema licha ya kuhamia katika chama cha CCM ataendelea kusema ukweli na
kuichukia rushwa na kwamba iwapo chama hicho hawatakubalina nae pia hatasita
kuhama tena na kwenda kwenye chama kingine.
Kwa upande wake Mwenyeiki wa chama hicho wilaya Moshi
vijijini Gabriel Masenga, alisema walikuwa ni wawajibikaji wazuri kiasi cha
kuitisha CCM na kwamba CCM wilayani humo itawatumia katika kuhakikisha
wanakijenga chama hicho na kuiimarisha imani waliyonayo wananchi kwa chama
hicho tawala.
No comments:
Post a Comment