KILIMANJARO jimbo la katoliki la mjini Moshi, wameamua kujenga shule ya walemavu
mchanganyiko katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
iliwaweze kusoma katika mazingira rafiki na waweze kupata elimu inayoenda sambamba na teknolojia ilikumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Akizungumza
na mwanaharakati wa mtandao huu Ofisini kwake Askofu mkuu wa
jimbo katoliki la Moshi Issac Amani, alisema ujenzi wa shule hiyo ya
sekondari ya watoto walemavu mchanganyiko ni wazo la kanisa hilo, baada ya kuona
watoto
wengi wenye mahitaji maalumu wakishindwa kuendelea na masomo ya juu.
Alisema kuna watoto wenye ulemavu na wana vipaji
mbalimbali na wanapochanguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, wanakutana na
changamoto za mazingira yasiyo rafiki ya kusomea na ukosefu wa waalimu wenye uwezo kitaaluma katika kuwafundisha watoto wenye
ulemavu.
Aidha
Askofu Amani
ameiomba jamii na taasisi mbalimbali kunga mkono juhudi za ujenzi wa
shule
hiyo, ili kuwasaidia watoto hao wenye ulemavu waweze kupata elimu nzuri, kama watoto wasiyo
na ulemavu.
Na kuwakumbusha watu wenye nafasi katika jamii kuwa na kila mmoja wetu atambue kuwa anawajibu wa kuisaidia jamii hususani yenye ulemavu na siyo kuiachia serikali peke yake.
Na kuwakumbusha watu wenye nafasi katika jamii kuwa na kila mmoja wetu atambue kuwa anawajibu wa kuisaidia jamii hususani yenye ulemavu na siyo kuiachia serikali peke yake.
No comments:
Post a Comment