KILIMANJARO serikali imetakiwa kuingialia kati tatizo la ulevi wilayani
Rombo mkoani Kilimanjaro kutokana na
tatizo hilo kuendela kushamiri na kuathiri nguvu kazi ya taifa ikiwa ni pamoja
na kuchangia ongezeko la watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Asasi ya jinsia na
maendeleo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro (AJIMARO) Athony Massawe, wakati
akikabidhi msaada wa chakula kwa watoto yatima na wale wenye maambukizi ya
ugonjwa wa UKIMWI katika kituo cha Cornel Ngaleku kilichopo wilayani humo.
Massawe alisema tatizo la ulevi kwa wananchi wilayani Rombo
limeendela kukua siku hadi siku na kwamba ni vema serikali ikaingilia kati na kulidhibiti, kwani limechangia maambukizi
ya ugonjwa wa UKIMWI na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wale waishio
katika mazingira magumu.
Aidha tatizo hilo limechangia kiwango cha umasikini
kuongezeka kwa wananchi wa wilaya hiyo kutokana na vijana wengi ambao ndio
nguvu kazi kuathiriwa na pombe hizo kali
na kusahau kufanya kazi kwa ajili ya kujileta maendeleo na kuondokana na
hali ya umasikini.
Massawe alisema kutokana na tatizo hilo asasi hiyo imejikita
katika utoaji wa elimu kwa wananchi juu
ya adhari za ulevi ikiwa ni pamoja na namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa
wa UKIMWI ili kuinusuru jamii hiyo.
Katika hatua nyingine Massawe aliitaka jamii, taasisi
mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuguswa na kuona umuhimu
wa kuwasaidia watoto yatima na wale
waishio katika mazingira magumu kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ukosefu wa chakula.
Awali akizungumza wakati akikabidhiwa msaada wa chakula hicho
Sista Ritha Massawe alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa chakula kwaajili ya watoto kutokana na wafadhili wengi
kuacha kutoa misaada kutokana na hali ya uchumi kuwa mbaya.
Alisema kwa sasa watoto yatima wengi wameongezeka ikiwa ni
pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu hali ambayo inachangiwa na ukosefu wa malezi bora kutoka kwa wazazi wao kutokana na kuendekeza ulevi hivyo kusahau wajibu wao muhimu.
Alisema wazazi wengi wameathiriwa na ulevi jambo ambalo
limekuwa likiwaathiri watoto ndani ya
familia na kupelekea watoto kutoroka majumbani na kuishi mitaani na kukosa
mahitaji muhimu kama chakula, elimu, mavazi na malezi bora.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wilayani Rombo walisema
kwasasa wanawake ndio wanaofanyakazi kutokana na vijana na wanaume kushindwa
kufanyakazi kwaajili ya kujiingizia kipato na kwamba wengi huishia vijiweni
wakivuta dawa za kulevya na kutumia pombe kali.
No comments:
Post a Comment