KILIMANJARO, Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro wamekamata ng’ombe zaidi ya elfu kumi ambao
wameingizwa kwenye shamba linalomilikiwa na mwekezaji Peter Jones, la Ndarakway,
lililoko kijiji cha Mitimirefu wilayani
Siha mkoani hapa.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, amesema ng’ombe hao wamekamatwa wakitokea
wilaya ya Longido, Siha na nchi jirani ya Kenya ambao waliingizwa na wafugaji
wa jamii ya Kimaasai kinyume na taratibu.
Gama amesema tayari uongozi wa mkoa huo, umeongeza askari wa kikosi cha
kutuliza ghasia ili kukabiliana na kundi kubwa la wafugaji hao ambao wameshindwa kutii amri ya
serikali inayowazuia kuingiza mifugo katika eneo hilo la mwekezaji huyo.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa mkoa, ameongeza kusema kuwa baada ya askari wa
kutulisa ghasia kufika katika eneo la mwekezaji huyo wafugaji hao
walitelekeza mifugo yao na kukimbilia
mapori , na kwamba Jeshi hilo
linaendelea na msako mkali ili kuwakamata wamiliki wa mifugo hyo.
Amefafanua kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imeongeza nguvu kwa
kuwapeleka askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), ili kukabiliana na
wafugaji hao ambao licha ya kutoa amri inayowakataza kuingiza mifugo katika
eneo hilo bado wafugaji hao wameshindwa kutii agizo hilo
Itakumbukwa kuwa novemba 21 mwaka huu
wafugaji wa jamii ya Kimaasai kutoka
nchi jirani ya Kenya na wilaya ya Longido, walivamia shamba la mwekezaji huyo na
kuteketeza nyumba kumi na sita na magari tisa wakidai eneo la malisho ya mifugo
yao.
No comments:
Post a Comment