KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imewataka watumishi wa shirika la TANESCO, kufanya kazi kwa uadilifu
ili kuzidisha ufanisi katika shirika hilo.
Hayo
yalizungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, wakati wa sherehe za
shirika hilo za kupongezana kwa kuvuka malengo ya kuwaunganishia umeme wateja
wake mkoani Kilimanjaro.
Gama
alisema TANESCO inaweza kufanikiwa
malengo yake kama watendaji kazi wake watakuwa waadilifu na waaminifu , na kuongeza kuwa ni vigumu kupata
mafanikio, kama watendaji hawata simama kwenye nafasi zao na kutimiza wajibu wao
ipasavyo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Umeme
nchini (TANESCO), Felschesmi Mramba, amewataka wafanyakazi wa shirika hilo
kubadilika kiutendeji kazi hatua ambayo itawawezesha kwenda na kasi ya mahitaji ya wateja ambao
wanahitaji huduma hiyo.
Mramba
alisema haiwezekani Tanzania ikawa nchi iliyoendelea kama wananchi wake wote
hawatakuwa na huduma ya umeme.
Alisema
mabadiliko ya kweli ni lazima yaanzie kwa watendaji wake, na kwamba shirika
likibadilika litaibadilisha nchi, na tutakuwa na uchumi imara.
Aidha
aliongeza kusema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la wateja ambapo katika miaka
ya themanini walikuwepo wateja laki mbili tu lakini hadi kufikia mwaka huu 2014
wameongezeka na kufikia wateja 1.5.
No comments:
Post a Comment