KILIMANJARO utekelezaji wa agizo la Rais la kuzitaka halmashauri za wilaya
kujenga maabara za masomo ya katika
shule za sekondari za kata nchini, limeoneka kusuasua katika wilaya za Moshi
Vijiji, Hai na Same mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, aliyasema hayo jana
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
juu ya hali ya utekelezaji wa agizo hilo katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema ujenzi wa maabara katika shule za kata za wilaya hizo
unaendelea kusuasua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo muako mdogo wa wananchi wa uchangiaji wa fedha
za ujenzi wa maabara katika maeneo hayo.
Aidha alisema mpaka sasa zaidi ya maabara 497 zipo katika
hatua za mwisho za ujenzi katika shule mbalimbali za mkoa wa Kilimanjaro na
kwamba mahitahiji ya mkoani ni zaidi ya maabara 651.
Gama alisema zaidi ya shule 217 za sekondari za kata hazina maabara na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wakutosha
katika uchangiaji wa maabara ili kufanikisha malengo ya serikali ya kuinua
ufaulu wa masomo ya Sayansi.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema ujenzi wa
shule za sekondari za vipaji maalumu katika
masomo ya sayansi umekwisha kamilika katika wilaya zote na kwamba mwaka 2015
zitaanza kuchagua wanafunzi tayari kwa kuanza masomo.
Alisema shule hizo zitakuwa na kidato cha kwanza hadi kidato
cha sita na ambapo zitakuwa ni za bweni na zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi
kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment