Mkuu wa Biashara wa Fastjet Lan Petrie (kulia), akizungumza katika semina hiyo.
Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia), akizungumza katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, iliyohusu kuongezeka kwa safari za ndege za shirika hilo kila siku kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Ofisa Mtendaji wa Masula ya Biashara wa Fastjet, David Chacha, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari katika semina hiyo.
Ofisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza kwenye semina hiyo.
Hapa semina ikiendelea.
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya
wateja Fastjet, Kampuni ya ndege ya Kiafrika yenye gharama
nafuu imeongeza safari zake za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwenda Johanessburg Afrika Kusini.
Safari hizo ambazo hivi sasa
zitafanyika kila siku zimepangwa kwa kuwapa abiria fursa zaidi na
njia mwafaka na mbadala kwa nauli wanayoimudu.
Utaratibu huo mpya wa safari za
Johannesburg utaanza kufanya Oktoba Mosi, 2015 na tiketi kwa ajili
ya safari tayari zimeshaanza kuuzwa, ambapo nauli hizo
zinaanzia kiwango cha chini cha dola za Marekani 50 kwa safari ya
njia moja, bila kujumuisha gharama za uwanja na tozo za serikali.
Akitangaza safari hizo mpya Meneja
Mkuu wa Fastjet Kanda ya Afrika Mashariki tawi la Tanzania Jimmy Kibati alisema
kwamba kuongezeka kwa safari kupo sambamba na sera za kampuni hiyo
za mwitiko kwa mahitaji ya wateja.
“Kila mara tunaahidi kuongeza
kuongeza masafa kwenye safari zetu na hasa wateja wanapozihitaji,” alisema
Kibati akibainisha kwamba kuongezeka kwa masafa
kumesisitizia jukumu la Fastjet Tanzania kukua kwenye mtandao
wake kikanda, kuufanya usafiri wa anga kuwa rahisi, salama pia waumudu.
Kibati aliongeza kusema
kuwa kuongezeka kwa utaratibu huo pia kumetoa
uwezekano wa kuingiza ndege ya ziada kwenye
usafiri wa Tanzania baadaye mwezi huu na hivyo kufanya
idadi ya ndege A319 kufikia nne.
“Ukweli tunafurahi kwa mapokeo haya
chanya ambayo Fastjet imeshayapata ndani ya Tanzania na kwa nchi
jirani ambako inafanya safari zake,” alisema Kibati.
“Kwa kutumia gharama nafuu, Fastjet
zinaifanya usafiri wa anga kufikiw akwa urahisi kuliko ilivyokuwa
awali, ambapo abiria wetu wengi wanakuwa wasafairi wa kwanza ambao
kama sio hivyo wasingeweza kusafiri kwa njia ya anga,” alisema Kibati.
Utaratibu huu mpya
unafuatia kutangazwa hivi karibuni uendeshaji ambapo
ilitangaza kuwa na idadei kubwa ya abiria kwa mwenzi.
Katika kipindi
cha Julai, Fastjet ilisafirisha jumla ya abiria 71,763
ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 ikilinganishwa na kipindi cha Julai mwaka
jana. Jumla ya mzigo uliosafirishwa kwa mwezi Julai ulikuwa ni
sawa na asilimia 72 na kiwango cha kuwahi kilikuwa cha juu kwa asilimia 95 ya
kuwasili kwa muda unaotakiwa.
Njia ya Johanessburg ambayo
inajumuisha Harare, Zimbabwe na Lusaka Zambai hivi sasa zitawapa
wateja wake njia mbadala ya ziada kwa kusafiri kwa urahisi kwenda na
kurudi kwenye maeneo yao.
Fastjet pia imeongeza mara mbili masafa
yake kwenye njia mpya iliyozsinduliwa hivi karibuni ya Dar es Salaam
- Lilongwe kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki, ambayo
imefuatiwa sio muda mrefu tangu kuanza kwa safari zake kati ya miji
hiyo miwili Julai 29, 2015. Njia ya Dar es Salaam
na Kilimanjaro kwenda Entebbe zinabakia kuwa ni safari tatu kwa
wiki.
Tiketi unaweza kufanywa kwa
njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.fastjet.com,
kupitia ofisi za fastjet kwa saa 24 au kupiga simu namba +255
784 108 900, na malipo yanaweza kufanyika kwa fedha taslim au kupitia kwenye
mitandao ya simu ya Mpesa na Tigopesa.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
No comments:
Post a Comment