Mh, Davis Mosha akiwahutubia mamia ya waBondeniazi wa kata ya kata ya Bondeni. |
Ikiwa zimesalia Takribani siku ishirini na tisa kuweza
kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mgombea Ubunge
kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (ccm) Jimbo la Moshi Mjini Ndugu Davis Elisa
Mosha amezidi kumtesa Mpinzani wake kutoka Kambi Pinzani ya Ukawa anayesimama
kwa Tiketi ya Chadema Ndugu. Jafary Michael. Hayo yamedhihirika leo katika
Mkutano wa Hadhara wa Mh. Davis Mosha katika viwanja vya Manyema vilivyopo kata
ya Bondeni.
Meneja Kampeni wa Mh. Davis Mosha h. Mwita akizungumza na wakazi wa Kata ya Bondeni. |
Mkutano huo uliofurika mamia ya wakazi wa katahiyo huku
wakionesha furaha ya waziwazi, Wakazi wa Kata hiyo wamesema hawawezi kufanya
makosa tena katika kusimamisha Mbunge wa Jimbo la Moshi na watachagua Kingozi
sahihi ambaye ni Davis Mosha.
Wakazi wa kata ya Bondeni wakimsikiliza Mh. Davis Mosha akinadi Sera zake za maendeleo ya Moshi Mjini. |
Akizungumza kwa Furaha huku akiwa na Picha ya Mh. Davis
Mosha Bi. Veronica Deus alisema kama ni
kiongozi basi Mungu kawaletea Davis Mosha na atampigia kura na atahakikisha
analinda kitambulisho chake cha kupiga kura ili aweze kukitumia kumpeleka Davis
Mosha Bungeni ili alete Maendeleo. “Unajua huyu kijana Katosheka, Tayari ana
fedha zake na Desturi yetu hatuwezi chagua Fukara asiye na fedha, Ndio maana
tulimchagua Ndesamburo sababu ana Pesa, Sasa leo unaweza kumfananishaje Jafary
na Davis Mosha, Hii ni sawa na Kifo na Usingizi” Alisema Bi Veronica deus.
Mh. Davis Mosha akizungumza na Wakazi wa Kata ya Bondeni |
Pamoja na yote Mh. Davis Mosha alisema huu ni wakati wa
kufanya vitendo na si maneno ya siasa, Yeye si mwanasiasa ila ni mtendaji na
amekuja kushirikiana na wana Moshii kuijenga Moshi tunayoitegemea. “Huu si
wakati wa Kulala ni wakati wa Kufanya kweli, Tujumuike Pamoja kufanya kweli
kuiondoa chadema tumewapa nafasi muda mrefu na wametumia Halmashauri ya Moshi
Mjini kujinufaisha wao. Sasa ni zamuya Wananch I kula matunda ya kodi zao na
hakuna mwingine mwenye uwezo huo. Nitumeni mimi” Alisema Mh. Davis Mosha huku
akishangiliwa na ummati mkubwa wa watu.
Mke wa Mh. Davis Mosha Madame Nance akisalimu wakazi wa Kata ya Bondeni. |
Mh. Davis Mosha akiwaaga wakazi wa Kata ya Bondeni baada ya kumalizika kwa mkutano. |
No comments:
Post a Comment