Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 9, 2012

HALI ILIVYOKUA MOSHI KATIKA MATOKEO YA WALIOLAMBA AJIRA YA SENSA...!

Kamati ya sensa Kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangaza Ajira ya Makarani/Karani Msaidizi wa Sensa na iliwalazimu wanaotaka ajira kuweza kujaza fomu ambayo waliitoa katika Ofisi za kata, Na moja ya Viambatanishi vya Maombi hayo ilikua ni nakala ya vyeti, Mdhamini pamoja na Picha ya Muhusika.
WAKAZI WAMOSHI WAKITAFUTA MAJINA YAO

Hali ilikua Tofauti siku ya Leo ndani ya Manispaa ya Moshi Baada ya Usiku wa jana Gari ilipita ikitangaza na kuwajulisha walioomba wapitie Mbao za Matangazo zilizoko Manispaa na Kwa Mkuu wa Wilaya Moshi na walimu watakaokua wamechaguliwa waende kwenye semina ambayo ingeanza Saa mbili asubuhi katika Ukumbi wa Mawenzi sekondari siku hiyohiyo.

Na kundi la pili ambalo ni lile la wasio watumishi wa umma wataanza mafunzo tarehe 18.

Asubuhi kundi kubwa la watu lilitembeleana kuweza kuona Bahati yao lakini waliambulia Idadi ndogo ya Waliopata bahati ya Ajira hiyo ambayo hailingani na Matarajio yao kutokana na wingi wa Barua za Maombi.

Watu mbalimbali waliweza kutoa Maoni yao na kusema inawezekanaje Mafunzo yaanze siku ambayo Matokeo ya maombi ya Ajira yametolewa.

Hii ndo changamoto iliyoko katika Mchakato wa Sensa kwa Manispaa ya Moshi,

Tupe Taarifa na huko kwenu Uchaguzi wa watendaji ulikuwa vipi?


No comments:

Post a Comment