THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete kuwasili Ghana leo
kumzika Rais Mills
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa
miongoni mwa wakuu wa nchi 16 na wageni wengine wengi maarufu, akiwamo Waziri
wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mheshimiwa Hillary Clinton, kushiriki mazishi ya
aliyekuwa Rais wa Ghana, Mheshimiwa John
Evans Atta Mills kesho , Ijumaa, Agosti 10, 2012, mjini Accra.
Rais
Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kuwasili mjini Accra, mji mkuu wa Ghana,
adhuhuri ya leo, Alhamisi, Agosti 9, 2012, kuhudhuria mazishi ya kiongozi huyo
aliyefariki dunia mchana wa Jumanne, Julai 24, 2012 kwa ugonjwa wa kansa ya koo
kwenye Hospitali ya kijeshi inayoitwa 37 Military Hospital mjini Accra.
Rais
Mills ambaye amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 69 anatarajiwa kuzikwa kwenye makaburi yaliyoko eneo la bustani
la Geese kwenye Mtaa wa Castle Drive karibu na Hekalu ya Osu mjini Accra baada
ya kuwa mwili wake umeagwa kwenye shughuli maalum itakayofanyika kwenye bustani
ya Independence Square kesho Ijumaa.
Rais
Mills ambaye nafasi yake imechukuliwa na Rais John Dramani Makama atazikwa
katika kaburi lililojengwa na kampuni ya ujenzi ya Serikali ya China ya HL
Construction. Mwili utazikwa baada ya kupitishwa katika mitaa maarufu ya jiji
la Accra ili kutoa nafasi ya mwisho kwa wananchi wa Ghana kuuona na kuuaga
mwili huo kwa mara ya mwisho.
Jana,
Jumatano, Agosti 8, 2012, mwili wa Mheshimiwa Mills ulihamishwa kutoka kwenye
Hospitali ya 37 ya Jeshi la Ghana ambako umekuwa umehifadhiwa tokea kufariki
dunia na kupelekwa kwenye nyumba ya familia iliyoko katika Barabara ya Spintex
kwa ajili ya kufanyiwa taratibu za mila.
Baada
ya shughuli hiyo, mwili wa Mheshimiwa Mills ulihamishiwa kwenye jumba la kulia
la Ikulu ya Ghana ambako wananchi wamekuwa wanatoa salamu zao za mwisho kwa
mwili wa kiongozi wao. Mwili wa Rais Mills utabakia katika sehemu hiyo mpaka
utakapohamishiwa Independence Square kwa ajili ya shughuli ya mazishi.
Miongoni
mwa watu waliotoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais leo ni pamoja na Rais
John Kuffor ambaye Rais Mills alichukua madaraka kutoka kwake. Vikundi vya muziki
na vikundi vya utamaduni viliendelea kutumbukiza Ikulu siku nzima jana na usiku
kucha.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
8 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment