Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 25, 2012

HII HAPA SERENGETI FIESTA 2012 MOSHI...!

Kilimanjaro ndio mkoa ambao Serengeti Fiesta 2012 imeanzia. Tamasha hilo kubwa limefanyika usiku wa tarehe 24 kuamkia 25 August, kwenye uwanja wa chuo cha ushirika.
Tamasha hilo limepambwa na wasanii kama Prezo kutoka Kenya, Mwana FA, Joh makini, Shettah, Mr. Nice, Bob Junior, King Zilla, Stamina, Linah, Jambo Squad,  Rich mavoko,Nuru, Rachael, Juma Nature, na wengine wengi, bila kuwa sahau waigizaji wa filamu za Bongo (Ray Kigosi, Wema Sepetu, Anti Ezekeil, JB na Steve Nyerere.

Mr. Nice akiwa kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 na wachza show wake wakionyesha kuwa msiki ni sawa na baiskeli ukishajua umejua na huwezi tena kusahau.


Jambo squad wakilitawala jukwaa na style yao ya kuinamisha kichwa na kuweka mikono nyuma huku wakizunguka na kuzidisha burudani kwa mashabiki. Hawa jamaa wanatokea Arusha na nyimbo yao iliyowaweka kwenye ramani ya mziki ni "DISCO MALAPA" katika kuonyesha kuwa mziki wanaufahamu wakaja na nyimbo yao ya "MAMONG'O"


Huyu ndio Shetah akizitendea haki nyimbo zake juu ya jukwaa la Serengeti fiesta 2012.


Kijana kutoka Morogoro "Stamina" ni kati ya vijana wachache wanaotokea Morogoro ambao wanautendea mziki wa Hip Pop haki kwa kweli.


Rich Mavoko, na sox zake kama mchezaji wa mpira lakini ndio hivyo yupo jukwaani katika kuhakikisha anaendelea kuwapa mashabiki wake burudani kwa style tofauti tofauti.

 
Huyu ndio ndege mnana mwanadada ambaye anatokea THT anafamika kwa jina la Lina akiwa jukwaani akiwapa burudani wakazi wa Moshi na vitongaji vyake.

 
Lina alilitendea haki jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 hadi kuwanyanyua mashabiki na kwenda kumtunza, jukwaani yupo Ray, Anti Ezekiel na Steve Nyerere wakijaribu kumfuta jasho kwa pesa...

 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipanda jukwaani kuzindua rasmi Serengeti Fiesta 2012 na kumkabidhi gari mshindi aliyejishindia gari aina ya Vitz.


 Huyu ndio mshindi wa Gari aina ya Vitz kwenye shndano la Serengeti Fiesta 2012 anafahamika kwa jina la Adam.


Kulia ni Wema Sepetu akiwa na Ray Kigosi wakisherekea Fiesta na wakazi wa Moshi ikiwa ni pamoja na kutafuta watu wenye vipaji vya kuigiza ili waweze kuwaendeleza.


Mwana FA akiwaburudisha wakazi wa Moshi kwa kuwarudisha enzi za "lakini alikufa kwa ngoma" "mimi na demu dam dama" mpaka sasa mwana FA alizidi kuwadhihirishia wote waliofika kwenye Fiesta kuwa habahatishi mziki.


Mshiriki namba mbili kwenye shindano la Big Brother Afrika 2012 "Prezo" naye alikuwa juu ya jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 katika kuhakikisha wakazi wa Moshi wanaburudika.


 Mwanadada Rachel akiwa jukwaani akiwakosha wakazi wa Moshi kwa style yake ya kuimba na kucheza kwa ufanisi mkubwa.

 
Mwamba wa kaskazini ndio anavyo jiita na kwenye Jukwaa la Serengeti fiesta aliweza kuwatendea  mashabiki wake haki kwa kuwapa burudani mwanzo mwisho..


Muite kibla matata au Juma Kiroboto ndio alifunga jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 Moshi, hapo jukwaani ni Juma Nature akiwa na Stopa Rhymes mzee wa "Style tatu ndani ya track moja" 

Lakini mbele ya Camera/Jukwaa kulikuwa kuna mambo yanaendelea kwa wakazi wa Moshi.

Wakazi wengi wa Kaskazioni watakuwa wanamfahamu Teacher Steve (aliyechuchumaa) akijisahaulisha machungu ya mgomo wa walimu ndani ya Fiesta.


MC wa muda mrefu sana kwa watu wa kaskazini watakuwa wanamfahamu Sijabu nae alikuwa ndani ya Fiesta.

 
Vijana wa chuo cha ushirika hawakuwa nyuma katika kuhakikisha wanapata burudani kwenye kiwanja cha nyumbani, Kulia ni Innocent akiwa na mshaji wake Nicolaus.