Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 25, 2012

Kamanda Kova apata kigugumizi kumzungumzia kisa cha Dr. Ulimboka...!

  


KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesita kuelezea hatua walizofikia katika uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Stephen Ulimboka.

Juzi Kova aliahidi kuzungumzia suala hilo jana, lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kwamba ameshindwa kufanya hivyo baada ya polisi Makao Makuu kufanya mkutano kama huo na kuzungumzia juu ya sensa ya watu na makazi.

“Siwezi kuzungumza chochote kwani tayari polisi makao makuu leo wameitisha mkutano na vyombo vya habari na wanazungumza mambo mengine muhimu,” alisema Kamanda Kova.

Hata hivyo, Kamanda Kova kwenye mazungumzo yake, aliashiria kuwa mkutano huo utakuwapo lakini akasita kutaja siku ambayo atatekeleza ahadi hiyo.


Kamanda Kova juzi aliiambia Mwananchi kuwa, atazungumzia suala la Dk Ulimboka ili kuweka wazi kwa umma kuhusu tukio hilo lililokuwa gumzo katika siku za hivi karibuni.

Kamanda Kova alitoa kauli hiyo alipotakiwa na gazeti hili kueleza kuwa endapo Dk Ulimboka ni mmoja wa mashahidi katika kesi iliyokwishafunguliwa kuhusu tukio la kutekwa kwake.

“Tutazungumza na wananchi na wanahabari kwa ujumla kuhusu mambo mengine yanayohusu usalama wa nchi pamoja na hatua tulizofikia katika uchunguzi wa kitendo cha kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka,” alisema Kova.

 “Sisi tutaweka wazi wajibu tulioufanya na hatua tulizofikia kuhusu kutekwa kwake, mambo mengine ni ya kimahakama, hatuwezi kuyaingilia,” alisema Kova.

Dk Ulimboka ambaye anatajwa kuwa kinara wa mgomo wa madaktari, alitekwa usiku wa Julai 26 mwaka huu na kujeruhiwa vibaya, kisha kutelekezwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na tukio hilo, Daktari huyo wa Magonjwa ya binadamu alitibiwa kwa muda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Tangu arejee nchini, Dk Ulimboka amekuwa kimya na mara kadhaa akigoma kuzungumzia yaliyomtokea akisisitiza kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika.             Chanzo: Aidan Mhando

No comments:

Post a Comment