Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 20, 2012

KLABU ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro(MECKI) wafanya uchaguzi wa viongozi wapya na kupitisha katiba ya clabu...!

KLABU ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro(MECKI)imefanikiwa
kuipitisha rasimu ya katiba ya klabu hiyo sanjari na kufanya uchaguzi
mdogo wa viongozi wa ngazi za juu kutokana na viongozi waliokuwepo
kupangiwa majukumu mengine katika umoja wa vilabu vya waandishi wa
habari wa mikoani(UTPC)

Marekebisho hayo ya katiba yaliyofanyika chini ya tume maalumu
iliyoongozwa na mwenyekiti wake Hekton Chuwa na katibu wake Yusuph
Mazim ilimaliza kazi yake ya kukusanya maoni ya wanachama wa klabu
hiyo na kuyafikisha katika mkutano maalumu uliofanyika jana katika
ukumbi wa KNCU mjini Moshi

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa rasimu ya katiba ya klabu
hiyo,mwenyekiti wa tume hiyo ya marekebisho ya katiba Hekton Chuwa
aliwataka wanachama wa klabu hiyo pamoja na viongozi kuitumia katiba
hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Katika hatua nyingine wajumbe hao wa mkutano mkuu wamejaza nafasi
zilizokuwa wazi ambazo ni nafasi ya Mwenyekiti iliyochukuliwa na
Rodrick Mkundi  na nafasi ya katibu ambayo ilijazwa na Nakajumo James
ambapo nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilienda kwa Salome Kitomari na
nfasi ya Katibu msaidizi kunyakuliwa na Dickson Busagaga.

Aidha kufuatia Salome Kitomari awali kuwa mjumbe wa kamati kuu na
kuchaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti,nafasi yake
ilinyakuliwa na Neema  Kweka dhidi ya mpinzani wake Hawa Rashidi
ambapo kwa  upande wa nafasi ya Dickson Busagaga ilishindaniwa na
Samuel Shao dhidi ya Mpinzani wake Charles Lyimo ambapo Samuel Shao
aliibuka kidedea  n kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Mecki mkoani humo.

No comments:

Post a Comment