Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 17, 2012

UKATILI HUU DHIDI YA WANYONGE UTAENDELEA MPAKA LINI? ...!

 Mamalishe wa jijini Dar es salaam akiwa abebebwa juu juu.

Ninavyojua mimi ni kuwa mtu yeyote yule ana uhuru wa kufanya jambo lolote lile ilimradi tu asivunje sheria za nchi husika. 

 Kwa huyu mama ntilie kavunja sheria gani ikiwa mtanzania kama huyu hana elimu ya kuweza kupata ajira wala hana ujuzi wowote na hali halisi ya nchi ya tanzania inafahamika kuwa swala la ajira ni janga la kitaifa maana hata vijana waliomaliza vyuo vikuu wamekuwa wakipata shida sana kwenye swala la ajira. 

Mama huyu ameamua  kujikimu kimaisha kwa kufanya kazi ya mama lishe ili aweze kupata riziki yake yeye na familia yake.. Lakini cha ajabu askari wa jiji waliamua kuchukua sheria mikononi kwa kumzalilisha mama huyu kwa kumbeba juu juu kama jambazi, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi pia ni kinyume na haki za binadamu.

Wakati hali hii ya unyanyasaji ikiendelea kwa tabaka la chini, watanzania tulio wengi tunafahamu fika kuwa kuna Mafisadi, Walarushwa wakubwa, Majambazi wakubwa lakini hatujawai kuona wakibebwa juu juu kiasi hiki. 

Je hali hii itaendelea mpaka lini?
Mpo wapi watetezi wa haki za binadamu?
Mpo wapi watetezi wa wanyonge? 
Zipo wapi faida za wazawa wasio na mamlaka?  


No comments:

Post a Comment