Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 17, 2012

Mawaziri wa ECOWAS wakutana Abidjan kuijadili Mali ...!

 
viongozi wa jumuiya ya Ecowas wakiwa kwenye mkutano.

Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa Afrika Magharibi walikutana Jumatatu kujadili lini na jinsi ya kupeleka vikosi vya usalama kupambana na ghasia nchini Mali ambako wanamgambo wa kiislamu wamechukua udhibiti wa eneo la kaskaizini mwa nchi hiyo.

Jumuiya ya ECOWAS inajaribu kumaliza mizozo ya kisiasa  katika nchi zote za mali na Guinea Bissau ambako mapinduzi yalifanyika mwezi April.


Viongozi walikutana mjini  Abidjan nchini Ivory Coast kutathmini ombi la rais wa mpito wa mali Dioncounda Traore kuomba msaada wa kijeshi kupambana na waislamu wenye msimamo mkali na kuchukua tena udhibiti  upande wa kaskazini.


Mali imeomba msaada wa vifaa na usafiri wa anga lakini siyo wanajeshi .


Kabla ya mkutano msemaji wa ECOWAS  Sony Ugoh amesema viongozi wa eneo hilo wanasubiri mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kujadili kuhusu Mali kabla ya kuamua tarehe ya kupeleka wanajeshi. 

Chanzo: VOA

No comments:

Post a Comment