Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 19, 2012

NGAWAIYA AGOMA KUSAINI MATOKEO....!

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM,Mkoa wa Kilimanjaro Thomas Ngawaiya na wagombea wenzake watatu wamegomea kusaini matokeo ya uchaguzi wa CCM yaliyompa ushindi Jumanne Iddi.

Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama barabarani, James Kombe aliyepata kura 37 na mjumbe wa Kamati ya siasa na maadili ya mkoa wa Kilimanjaro, Mildred Kisamo, aliyeambulia kura 32.

Ngawaiya aliibuka na kura 267 wakati Idd Jumanne alipata kura 550 na kuwabwaga wagombea wenzake.

Wakati matokeo yanatangazwa, wagombea hao watatu hawakuwapo ndani ya ukumbi.

Baada ya kutanganzwa kwa matokeo hayo, Ngawaiya alidai uchaguzi haukuwa huru na haki kwani ulitawaliwa na kasoro nyingi.

Alisema malalamiko yao walishayafikisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, lakini cha kushangaza hayajakupatiwa ufumbuzi.

“Chakushangaza hata viongozi waliotoka Taifa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo nao hawakutaka kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko,” alisema Ngawaiya.

No comments:

Post a Comment