Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 23, 2012

Usafiri wa treni Dar kuanza mwisho wa mwezi huu..

Usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam unatarajia kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa ziara ya kukagua miundombinu itakayotumika kwenye usafiri huo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Kisamfu, alisema kuwa ziara hiyo ililenga kukagua vituo, mabehewa pamoja na matuta ili kuepuka ajali

Kisamfu alisema kuwa treni hiyo itakuwa na mabehewa sita ambayo yenye uwezo wa kuchukua watu 1,000. Alivitaja vituo ambavyo treni hiyo itakuwa inasimama kuwa ni Kamata, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Tabata Relini, Mabibo na Ubungo Maziwa.

Aidha, alisema kuwa tiketi kwa ajili ya treni hiyo zitatengenezwa na Kampuni ya Cellcom Wireless na kuwa zitakuwa zinauzwa kwenye vituo ambavyo treni hiyo itakuwa inasimama.

Kisamfu alisema kuwa kuna miundombinu bado haijakamilika, lakini pamoja na hayo usafiri huo utaanza kama ilivyopangwa huku ukarabati wa miundombinu mingine ukiendelea.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, aliwataka wananchi wote waliojenga pembezoni mwa reli kutoka mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake.

Aidha alilitaka TRL kuweka matuta pamoja na kuifanyia ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepusha ajali.

No comments:

Post a Comment