Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 2, 2013

Mfalme Mswatti: Wafanyabiashara wa Tanzania ongezeni thamani ya bidhaa..!

Mfalume Mswati III wa Swaziland akiingia katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimayaifa tayari kwa Uzinduzi Rasmi akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda.

Mfalme Mswatti wa Swaziland, amewataka wafanyabiashara wa nchini Tanzania kuongeza thamani ya bidhaa zao ili ziwe na ubora unaotakiwa na kushindana kwenye masoko ya kimataifa.
Mfalume Mswatti alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa anafungua Maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema iwapo maonyesho hayo yatatumika ipasavyo ni wazi kuwa wafanyabiashara watapata wasaa wa kutangaza biashara zao kimataifa na hivyo kujulikana ulimwenguni na kuyafikia masoko tarajiwa.

"Ili kuyafikia masoko ya kimataifa, ni lazima bidhaa ziwe na ubora unaotakiwa, tunaona Serikali ya Tanzania inawasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zinakubalika katika soko la ndani na nje, katika nchi yangu tunafanya hivyo," alisema Mfalme Mswatti.

Aidha, aliwashauri wafanyabiashara hao kutumia teknolojia ya mawasiliano kujitangaza kimataifa kwa maonyesho hayo na mengine kwani ndiyo uwanja pekee wa wafanyabiashara kujinadi kwa wateja wao.

Mfalume Mswatti aliwakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania katika maonyesho ya mwaka ya kimataifa ya nchi kwake na kukuza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Alibainisha kuwa ili nchi za Afrika zipige hatua kubwa kiuchumi, ni lazima kuimarisha ushirikiano baina ya nchi na nchi ili kujenga bara imara linalojitegemea kiuchumi.

Awali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, alisema idadi ya washiriki wa maonyesho hayo imeongezeka kutoka 1,341 hadi 1,600 mwaka huu, wakati kampuni za kimataifa zimeongezeka kutoka 11 hadi 32 mwaka huu.

Alizitaja changamoto zilizojitokeza kuwa ni nafasi finyu kwenye eneo la maonyesho na katika utatuzi wake alisema wizara yake imejipanga kwa kuongeza eneo.

Baada ya kufungua maonyesho hayo, Mfalme Mswatti, alitembelea mabanda manne ya Maliasili na Utalii,  Chuo cha Tiba Muhimbili,   Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) na banda la Kampuni ya Simu nchini (TTCL).

No comments:

Post a Comment