Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 2, 2013

Mke wa Obama awakumbuka waliokufa mlipuko wa bomu..!

Michelle Obama akiwa na Mama Salma Kikwete katika Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni, jijini Dar es Salaam jana.

Mke wa Rais Obama, Michelle Obama, ameweka shada la maua katika Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni, jijini Dar es Salaam, eneo yalipo mabaki ya waliokufa kwenye mlipuko wa bomu katika Ubalozi wa Marekani nchini, Agosti 7, 1998.
Michelle na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, waliweka mashada hayo ya maua baada ya kukabidhiwa na watoto wawili wa kike waliokuwa wamesimama eneo hilo maalum kwa ajili ya tukio hilo.

Mbali na kuweka mashada hayo, pia Michelle alipata fursa ya kushuhudia michezo mbalimbali, ikiwamo ya sarakasi na ngoma iliyofanywa na kikundi cha sanaa cha Baba watoto kwenye makumbusho hayo.

Baadhi ya majina ya waliofariki kwenye mlipuko huo wa bomu na kuandikwa kwenye kibao katika eneo hilo, ni  Abdurahman Abdalah, Ramadhan Mahundi, Abdallah Mnyola, Abbas Mwila na Yusuf Ndange.

Wengine ni Bakari Nyumbu, Mtendeje Rajabu, Dotto Ramadhan, Rogath Saidi, Hassan Siad na Aimosaria Mzee.

Baadhi ya vifaa vilivyokuwapo katika eneo hilo la kumbukumbu ni pamoja na mabaki ya baskeli, pikipiki na vinyago vya nyuso za wanadamu kuwakilisha waliofariki kutokana na mlipuko huo wa bomu.

Jiwe la msingi la kumbukumbu hiyo liliwekwa na Balozi wa Marekani wakati huo, Charles Stith.

Aidha kabla ya kuwasili kwenye makumbusho hayo, Michelle alitembelea ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) zinazoongozwa na Mama Salma Kikwete, jijini Dar es Salaam.

Akiwa hapo alipata fursa ya kusaini kwenye kitabu cha wageni, kupiga picha ya pamoja na mwenyeji wake na kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma.

No comments:

Post a Comment