Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 16, 2013

SHUHUDIA PICHA ZA MASHINDANO YA MAGARI NA PIKIPIKI MKOANI KILIMANJARO

MOSHI jana katika uwanja wa memorial uliiopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kulikua na furaha ya aina yake kwa wakazi wa mkoa huop na wale waliotoka mikoa ya jirani kwa kuweza kushuhudia mashindano ya magari na pikipiki.

Mashindano hayo yaliyo andaliwa na Kilimanjaro Motor Sports Club chini ya usimamizi wa Louis Bonzon ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana. Japo kulikua na changamoto za hapa na pale lakini waliweza kujitahidi kuweka mambo sawa na mashindano yakakamilika vizuri..

Kwa upande wa Magari washindi walikua kama ifuatavyo
1.Gurjit Singh Dhani / Karan Veer Singh Dhani / Moshi 6:12 
2. Robert Sander / Salma Sumra / Arusha 6:15 (4 sec penalty)
3. Salvatory Mcharo / Akram Hafidh/ Moshi 6:30
4. Louis Bonzon / Ahmed Hussein / Moshi 6:40
5. Faheem Aloo / Sharook Aloo/ Moshi 7:11
6. Gulam kasu / Joseph Devis / Moshi 7:40
7. Bob Taylor/ Zuber Kara / Dar ( DNF)

Pia kulikua na magari ya kawaida yaliyoshiriki katika mashindano na wao pia walifanikiwa kuonyesha uwezo wao na pia washindio walikua kama ifuatavyo:-
1. Shafin khan / Rahim Yakub (Arusha)
2. Kelvin Makoi / Shaushi Ayub / (Arusha)
3.Salim kamal / Raheem Yakub (Moshi)
4. Ruhlamin said / Furyaan (Moshi)
4. Goodluck Marua / Godfrey (Arusha)
4.Hari Mtui / Mustapha ally( Arusha)
4.Tito Jafary (Arusha)Washiriki wa mashindano ya pikipiki wakiwa tayari kuanza mashindano.Waendesha pikipiki ndio walivyo anza kuchuana vikali.


Hizi ni baadhi ya pikipiki mbili za washiriki zilizochelewa kuwaka ila baada ya sekunde chache walifanikiwa kuziwasha na kuendelea na mashindano.


Huyu ni kijana wa Moshi anayefahamika kwa jina la Kiduku aliyeweza kuwaongoza wenzake toka mwanzo wa mzunguko mpka alipokua akimalizia mzunguko wa mwisho akakanyaga jiwe na kuanguka, akashindwa kuendelea na mashindano na hapo ndipo alipowapa nafasi washiriki wengine kuweza kumpita na kuibuka washindi.

Hii ni gari aina ya Carina TI iliyoshiriki katika mashindano ya magari ya kawaida..


Gari aina ya Forester iliyoshiriki katika mashindano ya magari ya kawaida ikionyesha uwezo.Gari aina ya land cruiser iliyoshiriki katika mashindano ya magari ya kawaida


No comments:

Post a Comment