Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, May 2, 2014

KAMPUNI YA PANONE YAFUNIKA KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MKOANI KILIMANJARO..,



Meneja wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd ndugu Gido L. Marandu akiwa kashika kombe la Ushindi katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi.


Msafara wa Magari wa Kampuni ya Panone ukielekea katika viwanja vya Chuo cha ushirika Moshi kwenye sherehe za Mei Mosi.


Wafanyakazi wa Panone and Co. Ltd Wakiingia Uwanjani kw Maandamano.


Gari la Matangazo la Kampuni ya Panone likiingia Uwanjani.

Gari ambayo ni Mobile Sheli ikitoa huduma katika sherehe hizo.

Msafara wa Maandamano wa Panone Ukipita mbele ya Mgeni Rasmi.
Bi. Irine Afisa Masoko wa Kampuni ya Panone akimpatia Mgeni Rami ambaye ni Mkuu wa Mkoa Kilimanjao Mkate unaozalishwa na Kampuni ya Panone.


Mfanyakazi wa Panone akisalimiana na Viongozi baada ya kuwapatia zawadi ya Crips zinazozalishwa na Kampuni ya Panone.


Mfanyakazi wa Panone akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora toka kwa Mgeni Rasmi.


Vikombe vya washindi wa sikukuu za Mei mosi.



Mfanyakazi wa Panone akipokea kikombe cha ushidi kutoka kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya kampuni.



Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama Akizungumza na Wafanyakazi.

Panone and co. ltd na Ngiloi Ulomi Enterprises ni kampuni ambayo inajishughulisha na Uuzaji usambazaji na Usafirishaji wa Mafuta Katika nchi za Afrika Mashariki na Kati pamoja na Uuzaji wa wa vifaa vya magari kama Tairi, Betri za Magari na oil za magari.

Katika jitihada za kutoa huduma Bora, Kampuni ya Panone imejikuta ikiaminiwa na Mataifa mbalimbali. Kwa Tanzania Kampuni ya Panone ambayo makao yake makuu yapo Tabata jijini Dar es Salaam. Imeweza kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja na wamefanikiwa vema kuwa na vituo vya mafuta katika mikoa mbalimbali kama Pwani, Tanga, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Katika kila kituo cha Panone kuna supermarket ya Kisasa inayotoa huduma kwa Saa ishirini na nne. Huduma ya Kipesa na kibenki kupitia simu ya Mkononi ya M Pesa inapatikana kwa saa ishirini na nne.

Katika huduma ya mafuta kila mteja aapoweka mafuta katika kituo cha Panone anajaza Card maalum ya mteja ambayo inamuwezesha kupata zawadi ya Mafuta kila mwishoni mwa mwezi.Katika kuhakikisha jamii inapata bidhaa bora Panone imefungua Kiwanda cha mikate katika mkoa wa kilimanjaro na kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha mikate bora inayotambulika kama mikate ya Panone pia Kuna bidhaa ya Karanga, Korosho, Popcorn, Crips na kufanya parking ya Sukari na mchele vyenye Nembo ya Panone.

Kwa sasa kampuni ya Panone ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa Hotel ya kisasa iliyopo Arusha eneo la King'ori kilometa chache kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Hotel hiyo inayotambulika kama Panone Luxury Motel na Pia kuna hotel ya kisasa ambayo ipo Arusha eneo la Sakina kwa iddy inayotambulika kama Panone Garden Hotel.

Katika kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi Kampuni ya Panone ndani ya mkoa wa Kilimanjaro kupitia vituo vyake vilivyombo mkoani Kilimanjaro ambavyo ni Same, Chekereni, Market Moshi mjini, Karanga Moshi Mjini na Weruweru wilaya ya Hai. Katika sherehe hizo Panone iliweza kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kupitia chama cha wafanyakazi TUICO.Katika sherehe hizo za Meimosi zilizofanyika Jana katika viwanja vya Chuo cha ushirika Moshi zilihudhiriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Jeshi la polisi Kilimanjaro, na viongozi mbalimbali. Sherehe hizo zilitangulia na Maandamano kisha zikatolewa zawadi baada ya hotuba ya Mgeni Rasmina mwishoni ikawa ni zawadi za vikombe katika maeneo matatu makuu ambayo ni Uzalishaji,Huduma na Ushiriki Bora. Kampuni ya Panone iliweza kuibuka mshindi wa Pili wa Ushiriki Bora katika Maandamano, Uwasilishaji wa Kazi zake kwa wananchi. Hii inadhihirisha ni jinsi gani kampuni hii imejipanga katika kazi zake.

Meneja wa Panone kwa kanda ya Kaskazini ndugu Gido L. Marandu alisema kampuni ya Panone inapata mafanikio kutokana na Utendaji bora wa wafanyakazi na kampuni inahakikisha inawapatia mahitaji yao kwa wakati.

No comments:

Post a Comment