Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, May 8, 2014

WAFANYAKAZI ZAIDI YA 150 WA KIBO MATCH NA KIBO PAPER WAKOSESHWA AJIRA

Wafanyakazi zaidi ya 150 wa viwanda vya kutengeneza ya Viberiti, Kibo match na kiwanda cha kutengeneza karatasi cha Kibo Kibo Paper vyote viliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamesitishwa ajira zao baada ya mwekezaji kushindwa kuviendesha viwanda hivyo.

Wakiongea na waandishi wa habari, baada ya kufika katika kiwanda cha kutengeneza Viberiti cha Kibo match, baadhi ya wafanyakazi wamesema kuwa wamepewa barua ya kusimamishwa rasmi ajira zao, lakini wamekuwa wakizungshwa sana kuhusu malipo yao.

Wafanyakazi hao walikuwa kisubiri mafao yao kiwandani hapo wamesema hawaridhishwi na taarifa za mafao waliyo ambiwa kuwa watalipwa kwa kuwa ni madogo ukilinganisha na muda waliofanya kazi katika viwanda hivyo.

Bwana Angelbert Ngowi ni meneja rasilimali watu wa viwanda hivyo, ambaye alisema vimefungwa kutokana na kujiendesha kwa hasara na kwamba wafanyakzi wameshapewa barua za kusitishwa ajira zao na taratibu za malipo kwa waliokuwa wafanyakazi wa vianda hivyo yamesha kamilika.

Kwa upande wa katibu wa chama cha wafanyakazi na biashara TUICO, mkoani Kilimanjaro Bwana Renatus Chimola, alisema mwekezaji huyo ambaye ni raia wa Nigeria amesema atawalipa wafanyakazi haki zao zote kwa mujibu wa sheria na taratibu za kazi na kwamba baada ya mwekezaji kukamilisha malipo hayo viwanda hivyo vitauzwa ama kutafutiwa mwekezaji mwengine.

No comments:

Post a Comment