WAJUMBE wa bunge
la katiba, wametakiwa kuacha kutumia muda mrefu kujadili masuala ambayo hayana
tija kwa jamii, badala yake kujikita zaidi katika masuala ambayo
yatalisaidia taifa na jamii kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Askofu mkuu wa
dayosisi ya Mashariki na Pwani, Stanley Hotay, katika jubilee ya kuadhimisha
miaka 75, tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo na sherehe ambazo ziliendana
sambamba na harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa hilo.
Askofu Hotay amesema kanisa haliko tayari kuona kuna kuwepo na makundi
ya wawakilishi walioko ndani ya bunge la katiba wanakuwa wapiganaji ambao
wanahamamisha ubaguzi ndani ya Tanzania.
Askofu huyo amewataka wajumbe wa bunge la katiba
kuzingatia maadili na maamuzi yao yawe yenye tija kwa wananchi ili kuweza
kupatikana katiba iliyo na manufaa bora.
Hata Askofu Hotay, ameongeza kuwa,
wajumbe hao wanatakiwa kutambua kuwa wanatumia fedha za wananchi ambao ni wa
hali ya chini kulipwa posho zao huku wakiendelea kususia na kutoka ndani
ya bunge hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Anna Rose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo,
amewataka wananchi pamoja na viongozi wa dini kucha kushabikia wanasiasa
wenye lengo la kutumia mchakato wa upatianaji wakatiba mpya kuvuruga amani.
No comments:
Post a Comment