Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 17, 2014

JESHI LA POLISI TANZANIA LAJIPANGA KUJENGA KITUO KATIKA KILA TARAFA

JESHI la Polisi lina mpango kabambe wa kusogeza huduma ya ulinzi na usalama karibu na wananchi kwa kujenga angalau kituo kimoja cha polisi katika kila tarafa kwa upande wa Tanzania bara na jimbo kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira A. Silima amesema hayo jana bungeni mjini hapa wakati akijibu swali la mbunge wa Mbeya Vijjni mchungaji Luckson Mwanjale.

Katika swali lake mchungaji Mwanjale alitaka kujua lini Serikali itapeleka huduma kwenye tarafa ya Isangati na kama Serikali itakuwa kutafiti maeneo mengine ya kupeleka huduma hiyo.

Akijibu maswali hayo Silima amesema utekelezaji wa mpango huo unategemea fedha zitakavyotolewa na serikali kwenye bajeti ya mwaka hadi mwaka. 

Amefafanua  kuwa pindi fedha zitakapopatikana tarafa zote zitajengwa vituo vya polisi ikiwemo tarafa ya Isangati.


Aidha amesema jeshi la polisi linaendelea kubaini na kuyatambua maeneo mbalimbali ambayo yanahitaji kupelekewa miundombinu ya huduma ya ulinzi na usalama ikiwemo kujenga vituo vya polisi katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment