Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 3, 2014

TIMU YA PANONE FC YATANGAZWA BINGWA HUKO MBEYA...., KIKOSI CHA TIMU YA PANONE FC WAKIWA KATIKA PICHA KABLA MCHEZO WAO


Ligi Daraja la Pili ngazi ya Mikoa iliyokua ikitimua vumbi katika vituo vitatu ambavyo ni Mbeya, Shinyanga na Morogoro imehitimishwa hapo jana katika Mashindano ya Kutefuta timu ambazo zitaelekea katika ligi daraja la kwanza. Katika Kituo cha Mbeya kulikua na Takribani timu Tisa kutoka katika Mikoa Tisa ya Tanzania Bara ambapo Moja ya Mkoa uliopangiwa katika kituo hicho ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro uliowakilishwa na Timu ya Panone Fc.

Timu ya Panone Fc iliweza kushuka Dimbani hapo jana katika mchezo wao wa Mwisho Dhidi ya Timu ya Small Town ya Ruvuma ambapo mchezo huo ulipigwa saa Kumi kamili katika uwanja wa Vwawa wilaya ya Mbozi. Katika mchezo huo Timu ya Panone Fc ilihitaji Ushindi ili iweze kufuzu mashindano Huku nayo timu ya Njombe Mji ya Mkoa wa Njombe ikiwa inachuana na Timu ya AFC ya Arusha katika uwanja wa Mbeya Mjini huku Njombe wakiwa wanahitaji Ushindi na kuiombea Panone Fc ipoteze mchezo ili iweze Kushinda.

 WAAMUZI WA MCHEZO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MA KAPTENI WA TIMU.

Katika Mchezo hapo Jana Hali ilikua tofauti mnamo wa Dakika ya Tatu Mchezaji wa Panone Fc Ramadhan Hasan Aliweza kuiandikia Goli la Kwanza Timu yake na kuamsha Mashambulizi na Hari mpaka Dakika ya Sita ya Kipindi cha kwanza ndipo Ayoub Ruben alipoifungia Goli la Pili Timu ya Panone Fc na kuyazima matumaini ya Timu ya Small Town ya Ruvuma. Mpaka Mpra kuisha Panone Fc ilipata ushindi wa Goli mbili kwa bila dhidi ya Small Town ya Ruvuma huku Timu ya Njombe Mji na AFC ikitoka Sare ya Goi moja kwa moja na Matokeo hayo yakazima ndoto za Timu ya Njombe mji huku Nyota ya Panone Fc iking'ara.

 MA KAPTENI WA TIMU WAKIPATA MAELEKEZO TOKA KWA REFA KABLA YA MCHEZO KUANZA.

Kutokana na Ushindi huo Timu ya Panone Fc imeweza kupanda Daraja na kwenda Daraja la kwanza na kuufanya mkoa wa Kilimanjaro kupata Timu ambayo itashiriki Ligi Daraja la kwanza ambayo waliikosa kwa kipindi kirefu. Tulipata Fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd Ndugu Patrick Ngiloi Kupitia Kampuni yake ndio wanaoiwezesha timu hiyo aliweza kuzungumzia mafanikio ya timu hiyo huku akisema mafanikio hayo ni ya Mkoa wa kilimanjaro yeye kama mdau kupitia kampuni yake ameweza kuwaweka vijana pamoja na kujiajiri katika michezo na kuwaepusha na Uvutaji wa Dawa za kulevya na hata uhalifu na kujikita katika michezo na Heshima hii si ya Kampuni ya Panone Pekee ni heshima kwa Mkoa Mzima wa Kilimanjaro na Akawataka wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro waiunge mkono Timu hiyo iweze kufika mbali.

WACHEZAJI WA PANONE FC WAKISHANGILIA USHINDI BAADA YA MCHEZO

MASHABKI WAKIWA UWANJANI WAKIFURAHIA USHINDI PAMOJA NA WACHEZAJI

NI FURAHA TU.....,


No comments:

Post a Comment