Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, June 9, 2014

TUMBILI, NGEDERE NA NYANI WAWASABABISHIA WAKULIMA HASARA KUBWA

MOSHIA makundi makubwa ya wanyama aina ya Ngedere, Tumbili na Nyani wamevamiamashamba ya wananchi wa  vijiji vya Tella, Mbokomu, Kimochi na Sango na kula mazao yote hali ambayo wamedai ina ashiria kukumbwa na njaa kutokana na hali hiyo ya mazao waliokuwa wanayategemea kuliwa yakiwa shambani.

Wakazi hao ambao wamezungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti tofauti na kuonesha masikitiko makubwa sana,  wameiomba serikali kupitia  wizara ya maliasili na utalii kuwaagiza maaskari wa wanyamapori ili kwenda kuwawinda wanyama hao kutokana na wananchi hao kuzidiwa na wingi wa wanyama hao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, Ezron Macha, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Old moshi Magharibi amesema >> "wanyama hao wamevamia mashamba yake na kula mazao yakiwemo mahindi, ndizi, na maparachichi,
ambayo alitegemea kuanza kuvuna siku za hivi karibuni"


Naye Elisaria Raphael Mrema, amesema >> "Wanyama hao wamekuwa wakija kwa makundi makubwa na kuvamia mashamba na kuharibu mazao na taarifa hizo walisha  zifikisha kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili ili kuwa
saidia tatizo hilo la wanyama lakini hadi sasa hawajawaona watumishi hao kufika kijijini hapo"


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Halmashauri ya Moshi, Msami Mshana, amekiri kuwepo kwa makundi hayo ya wanyama na kusema kuwa hilo ni tatizo kubwa.

Mshana amesema wilaya ya Moshi ina vijiji 145, na kwamba Halmashauri pekee inao maaskari wa wanyama pori wawili, hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu kuyafikia maeneo yote  kutokana na uchache wa watumishi hao.

Hata hivyo Mshana ametoa wito kwa wananchi wenye Bunduki ambazo zimesajili kihalali kufika ofisini kwake ili kupata vibali cha kwenda kuwawinda wanyama hao.

No comments:

Post a Comment