Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 5, 2014

TAZAMA TIMU YA PANONE FC ILIVYOWASILI MJINI MOSHI...,
Timu ya Mpira wa Miguu Panone Fc ya Mkoani kilimanjaro iliyokua Ikiuwakilisha Mkoa kilimanjaro katika Michuano ya mashindano ya Mabingwa wa Mikoa katika ligi Daraja la Pili huko jijini Mbeya imewasili Jana jioni  katika Mkoa wa Kilimanjaro na Kupokewa mjini Moshi na wadau mbalimbali wa Michezo.
 Tazama Picha za Mapokezi ya Timu hiyo baada ya kurudi na Ushindi na kpelekea Mkoa wa Kilimanjaro upata timu itakayoshiriki ligi Daraja la Kwanza baada ya takriban miaka kumi na Tano kupita bila kuwa na Timu iliyofuzu kushiriki ligi Daraja la kwanza.
 
 


 Mtangazaji wa Habari za Michezo Akiwa na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Kilimanjaro pembeni ya Gari ya Matangazo wakisubiri kuipoea Timu nje kidogo ya mji wa Moshi.


Basi la Hood lililobeba wachezaji wa timu ya Panone Fc likiingia Moshi. 
Viongozi wa msafara wakiwa katika Basi pamoja na Kocha wa Panone Fc wakiingia Moshi kwa furaha.


Msafara wa Magari wa Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Kilimanjaro na waau wa Michezo wakiwa wanaongoza gari lililobeba wachezaji.


 Mchezaji wa Panone Fc akiwa amepozi katika Gari baada ya safari ndefu kutoka Jijini Mbeya

Mwenyekiti wa Paone Fc ndugu Simon Kajaus Akiangalia Mandhari ya Mji wa Moshi 

Msafara ukiwa unaingia katikati ya mji wa moshi

Basi la Hood Lililobeba wachezaji likiwa limeingia mjini moshi

Wachezaji wakishuka baada ya Kufika Mjini Moshi.

Meneja wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd Ndugu Gido Marandu akizungumza na Waandishi wa habari.

 Mwamuzi Mstaafu na Mmoja wa wanakamati waliokua katika msafara na Timu Ndugu Amri Kiula akifafanua jambo kwa viongozi wa chama cha mpira wa Miguu Kilimanjaro.

Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Kilimanjaro Wakisikiliza jambo kutoka kwa Amri Kiula {Hayupo pichani}

Baada ya Safari wachezaji walipata Fursa ya kupata chakula cha jioni pamoja na wadau wa michezo kaika mgahawa wa Fresh mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment