Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 26, 2014

WAZEE WASHAURIWA KUACHANA NA MATUMIZI YA POMBE NA SIGARA

HAI wazee wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuachana na matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara na kujiweka katika hali ya usafi ili waweze kuwa na afya bora na kuondokana na magonjwa yasiyo kuwa ya lazima.

Ushauri huo umetolewa na muuguzi toka hosipitali ya wilaya ya Hai Bi. Peliciana Ritte alipo kuwa katika semina ya usafi binafsi kwa wazee iliyo andaliwa na shirika la “Dorcus Aid International” iliyo fanyika katika kijiji cha cheki maji na kukutanisha wazee 196 toka vijiji nane vya wilayani Hai.


Bi. Rittel ilisema kuwa wazee wengi wamekuwa wakinyemelewa na magonjwa mbali mbali ikiwa sukari pamoja na presha na hata kupata haja kubwa kwa shida kutoka na na kukosa lishe bora na matumizi ya pombe kali na sigara jambo linalo wasumbua wazee wengi vijijini.


Alisema kuwa Jamii nyingi zimekuwa zikiwachukulia wazee kama mizigo hivyo kuwatelekeza bila msaada wowote jambo ambalo linafanya wazee hao kuendelea kuteseka kwakukosa uangalizi hali inayosababisha wazee wangi kuwa wachafu na wengine kujiingiza katika unywaji pombe na uvutaji sigara kitu ambacho kinafanya afya zao zizindi kuzorota.


Akizungumzia kuhusu matibabu alisema kuwa kila mzee anapaswa kufuata taratibu na kupata maelekezo toka kwa viongozi ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho kinacho tambulika au kuwa na bima ya afya ili kuweza kutibiwa kirahisi na kuondokana na lawama zinazo jitokeza katika kupata huduma.


Kwa upande wake mzee Abeli Daniel Mhina ameeleza kuwa wazee wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika kupata huduma licha ya kuorodhesha majina na kutambulika jambo ambalo lina wanyima haki zao za msingi kama serikali inavyo taka wazee kuhudumiwa.


Ameongeza jambo linguine linalo wakwamisha wazee kupata huduma za afya ni hali ngumu ya maisha pamoja na umbali wa kuzifikia hosipitali zinazotoa huduma kwa wazee na
  pengine kukosa madawa katika vituo hivyo.

Awali akitoa ufafanuzi wa kuanzishwa kwa shirika hilo la “Dorcus Aid International” mratibu wa shirika hilo Bw. Saimon Shoo ameeleza kuwa shirika hilo lilianzishwa mnamo mwaka 2006 likiwa na wazee 25 toka vijiji nane vikiwemo rundugai, chekereni, longoi, ngosero na vingine ni tindigani, mkalama, kawaya na kikavu chini ambapo hadi sasa idadi imeongezeka na kufikia 196 wake kwa waume huku 53 wakiwa wamekwisha fariki.


Bw. Shoo ameongeza kuwa shirika hilo linalenga kutoa huduma kwa wazee ikiwa ni pamoja na matibabu na kuwapa mahindi, unga wa lishe, sabuni, mara sita kwa mwaka na mafuta ya kupikia na mafuta ya kujipaka wakipewa mara tatu kwa mwaka.

Hivyo ameitaka serikali kushirikiana na mashirika mabilmbali kuwapa huduma bora wazee hao ikiwa ni pamoja na kuzidi kutenga maeneo rasmi ya  wazee kupata matibabu pamoja na kupunguza gharama za matibabu kwani matibabu kwa wazee yamekuwa ni makubwa.

No comments:

Post a Comment