Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa
katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao
kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana
jijini Arusha.
Majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional
Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25), akiwa amelazwa
katika hospitali ya Selian, katika chumba cha watu mahututi (ICU), mara
baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mguu huo
kujeruhiwa vibaya na bomu.
Sehemu
ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana
usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa
katika hospitali ya Selian, jijini Arusha kwa matibabu.
Uharibifu uliofanywa na bomu hilo.
Watu wanane wamejeruhiwa
usiku wa kuamkia leo baada kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kurushwa
katika mgahawa ujulikanao kama Vama uliopo katika jengo la club ya
gymkhana karibu na mahakama kuu ya mkoa wa Arusha.
Katika
tukio hilo lililotokea majira ya saa 4.30 usiku baada ya watu
wasijulikana wanaodaiwa kurusha kitu hicho kilichosababisha mlipuko
mkubwa ambao ulijeruhi baadhi ya wateja waliokuwepo katika mgahawa huo
ambapo majeruhi hao walikimbizwa katika hospitali ya seliani ya mjini
Arusha.
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa hospitali ya seliani dr.Paul Kisanga amethibitisha
kupokea majeruhi 8 kati yao wamo wanaume watano na wanawake 3 wakiwemo
watoto wawili wote raia wa Tanzania wenye asili ya Asia huku akimtaja
Deepack Gapla kuwa na hali mbaya ikiwa ni pamoja na kupoteza mguu mmoja
na hivi sasa yupo chini ya uangalizi maalum ICU.
Camera
yetu ilifika katika eneo la tukio na kukuta eneo hilo likiwa chini ya
uangalizi maalum wa askari jeshi la wananchi kitengo maalum cha
uchunguzi wa mabomu kwa kushirikiana na jeshi la polisi wakiendelea na
uchunguzi wa chanzo cha mlipuko huo ambapo waandishi wa habari
walipojaribu kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus
Sabas alikataa kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa suala hilo
litatolewa ufafanuzi makao makuu ya jeshi na mkurugenzi wa upelelezi
makosa ya jinai DCI Isaya Mghulu.
Picha kwa hisani ya Jiachie Blog.
No comments:
Post a Comment