Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 8, 2014

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA USHIRIKA NA BIASHARA (MUCCoBS) KUPANDISHWA HADHI NA KUWA CHUO KIKUU KAMILI

CHUO Kikuu kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCobs), kimesema kuwa kiko katika hatua za mwisho katika mchakato wa kupandishwa hadhi na kuwa chuo Kikuu kamili, cha Serikali cha kwanza kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine K. Bee, wakati wa hafla fupi uzinduzi wa serikali mpya ya wanafunzi wa chuo hicho, (MUSCO), sherehe ambazo zilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo hicho.

Profesa Bee amesema mchakato wa chuo hicho kuwa chuo Kikuu umefikia katika hatua za mwisho,  baada ya kufanyiwa tathmini na tume ya vyuo vikuu Tanzania,  tangu mwaka 2006, 2012 na mwaka 2014, na kujiridhisha kuwa na kiwango cha kwenda kuwa chuo Kikuu kamili.

Amesema kwa sasa chuo hicho kipo katika kuandaa mchakato wa wa kukipeleka kuwa chuo kikuu kamili kwa kuzingatia taratibu zilizopo, ambapo usajili kamili kilipewa tangu mwaka 2012.

Kwa upande wake Rais mpya wa (MUSCO), Rahim Msofe akitoa neno  la shukrani kwa wanachuo hao,  amewaomba viongozi wenzake waliochaguliwa kuwa watatoa ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa chuo hicho na kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na uongozi ambao umemaliza muda wake.

Amesema kazi kubwa iliyopo mbele yake ni kuhakikisha wanafunzi  wanapata bima ya afya ili kuweza kuwa na afya bora,  ikiwa ni pamoja na kushirikiana kwenye utekelezaji wa mipango ya MUCCObs kuwa chuo kikuu kamili..

No comments:

Post a Comment