Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 10, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - IFIKAPO NOVEMBA 20014 VYUMBA VYA MAABARA VIWE VIMEKAMILIKA



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Wananchi kuhakikisha kuwa ifikapo Mwezi Novemba Mwaka huu,  kila Shule ya Sekondari katika maeneo yao, ina  maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.
Rais Kikwete amesema hayo Mkoani Tanga katika nyakati tofauti Wilayani Kilindi na Lushoto ambapo yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Tanga tangu tarehe 8 Julai hadi tarehe 12 Julai,2014.
"Nataka ifikapo Mwezi Novemba, Mwaka huu vyumba vya maabara viwe vimekamilika, tulipeana miaka miwili, imetimia" Rais amesema na kuongeza kuwa lazima tusahihishe makosa tuliyofanywa ya kutojenga maabara wakati tunajenga shule za sekondari nchini kote.
Mwaka 2006, Serikali ilihamasisha ujenzi wa Shule za Sekondari nchini kote na muitikio ni mzuri, lakini hakukuwa na uhamasishaji wa kujenga maabara. “Tumeamua kushughulikia suala la maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya Sayansi kote nchini." Rais amesisitiza.
Rais amesema ameridhika na upanuzi wa Elimu katika ngazi za Msingi na Sekondari kote nchini na Serikali inaendelea na hatua ya kutatua changamoto za ubora wa Elimu, kuongeza Walimu, kuongeza Vitabu, ujenzi wa Maabara na Nyumba za Walimu kote nchini.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara Wilayani Lushoto Rais ameahidi kuboresha na kushughulikia suala la ujenzi wa barabara ya kwenda Bumbuli na zaidi kuhakikisha anaweka barabara ya lami katika mji wa Lushoto na mji mdogo wa Bumbuli.
Rais anaendelea na ziara Wilayani Lushoto na Mkinga ambapo anaendelea kuzindua miradi na kukagua miradi ya maendeleo.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Julai,2014

No comments:

Post a Comment