Vijana wanaopitia vyuo vya
elimu ya juu hapa nchini wametakiwa kuwa na ujasiri na kutumia vyema
fursa zinazotolewa na Diplomasia ya Uchumi, katika kukabiliana na
changamoto za ajira.
Wito
huo umetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka wakati alipokuwa akizungumza
kwenye kongamano la vijana wa elimu ya juu kuhusu kukuza Diplomasia ya
Uchumi.
Prof. Tibaijuka
amebainisha kwamba vijana wa Kitanzania wanaweza kupunguza changamoto
ya ukosefu wa ajira kupitia uhusiano na ushirikiano na vijana wenzao
kutoka mataifa mengine.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Mapinduzi Mkoa Maalumu wa vyuo
vya Elimu ya Juu ambapo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya
juu wameshiriki.
No comments:
Post a Comment