Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 6, 2014

JINSI YA KUKABILIANA NA KUANGUKA KWA VYAMA VYA MAZAO NCHINI TANZANIA

MOSHI imeelezwa kuwa kuanguka kwa vyama vya mazao hapa nchini vimesababishwa na vyama hivyo kutokukubaliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo kwa sasa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCobs),  Prof.  Faustine Bee, wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari ofisini kwake, ambapo amesema kuwa  sababu kubwa ya kuanguka kwa vyama hivyo vya mazao ni kutokutaka kubadidilika kwa mfumo wa kiuendeshaji wa mazao hayo.

Amesema ipo haja kwa vyama hivyo kuanza kufikiria usindikaji wa mazao ambayo ndiyo njia pekee ya kuweza kupata vyama vya ushirika imara ambayo vitaweza kumkomboa mkulima mdogo ili aweza kukabiliana na hali ya kiuchumi.

Amesema sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa elimu  ya ushirika miongoni mwa wanachama  hao,  na kwamba karibu asilimia 20 tu ya watanzania ndio ambao wananufaika na biashara ya ushirika hapa nchini.

Amesema  asilimia 55 hadi 60,  ya vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa vikifanya vizuri ni vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), na kwamba asilimia nyingine  ni vyama vya aina mbalimbali ikiwemo vyama vya mazao.

Aidha Prof. Bee amewataka wanafunzi wanaomaliza vyuo kuanzisha vyama vya ushirika vya  usindikaji wa mazao ambavyo vitawasaidia kujiajiri pasipo kutegemea ajira kutoka serikalini.

Kwa upande wake Rais wa wanafunzi wa (MUCCobs), Rahim Msofe, amewashauri vijana kujiunga katika vyama vya ushirika na kuacha tabia ya kutegemea ajira kutoka  serikalini.

Amesema  vijana ni vyema wakaanzisha vyama vya ushirika hali ambayo itasaidia kuendeleza jamii inayowazunguka ili kuleta maendeleo katika taifa.

No comments:

Post a Comment