KILIMANJARO kanisa la KKKT dayosisiya kaskazini limeanzisha mradi wa upatikanaji wa nishati inaotokana
na kinyesi cha ng’ombe kwajili ya matumizi
mbalimbali hususani ya kupikia mradi ambao utasaidia kupunguza kwa kiasi
kikubwa tatizo la uharibifiu wa
mazingira ususani ukataji wa miti .
Mradi huo umeanzishwa na KKKT kwa ushirikiano wa Tanzania domestic program kupitia
taasisi ya camatec ambapo wametoa elimu kwa wananchi kuachana na matumizi ya nishati itokanayo na miti na badala
yake watumie nishati itokanayo na kinyesi cha ng’ombe yaani (biogas), na tayari mitambo
150 imeshajengwa katika wilaya 5 za mkoa wa Kilimanjaro.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu
mkuu wa KKKT wa dayosisi hiyo Dr. Martin Shao, Wakati akizindua siku ya upandaji
miti katika kijiji cha nshara wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kwenye eneo linalo tarajiwa kujengwa machame kampasi
ya chuo kikuu cha kumbukumbu ya Askofu Stefano kinachomilikiwa na kanisa la KKKT.
Aidha Askofu Shayo amevipongeza
vijiji vya uronu, nshara na ufoo, kwa kulipatia kanisa
hilo eneo lenye ukubwa wa hekati 50 za ardhi kwaajili ya kujenga makao makuu ya
chuo hicho ambapo katika uzinduzi huo, baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliotesha
miti kuzunguka katika eneo hilo.
Mkuu wa chuo hicho Anold Temu amesema wakati mchakato wa ujenzi
huo ukiendelea chuo kitaanza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa waalimu wa shule mbalimbali
za sekondari na baada ya ujenzi kukamilika, kitatoa masomo ya shahada ya
sayansi kwa wanafunzi na waalimu hapa nchini na mataifa mbalimbali Duniani.
No comments:
Post a Comment