Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 4, 2014

MTOTO WA MIAKA 9 ALIYEPANDA MLIMA KILIMANJARO AWAHAMASISHA WATANZANIA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI


WATANZANIA wametakiwa kutumia utalii wa ndani ili kuwavutia watalii wengi kufika kwa wingi hapa nchini na kuweza kujionea vivutio na maliasili zilizopo hapa nchini na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Mtanzania wa kwanza mwanamke kupanda mlima Kilimanjaro, akiwa na umri wa miaka (9), Idda Baita, mwanafunzi wa darasa la nne, ambaye ameweka rekodi mpya katika historia ya upandaji wa mlima Kilimanjaro mlima mrefu barani Afrika kupitia njia ngumu ya Umbwe Kibosho na kufanikiwa kufika katika kilele hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuku mlimani, Idda alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa kwake na kutoa wito kwa wazazi kutembelea vivutio hivyo vilivyopo nchini ili kuweza kujifunza uhifadhi.

Alisema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuupanda mlima huo kama njia ya kuthibitisha uzalendo wake ambapo pia amesema atakuwa balozi katika kuwahamasisha vijana wenzake kupanda mlima Kilimanjaro hasa wanapokuwa likizo.

Kwa upande wake Muongoza watalii mlima Kilimanjaro, Respicious Baitwa, ametoa rai kwa wadau wote hasa watanzania kushiriki kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukuza utalii wa ndani .

Baitwa alisema jamii imekuwa na mawazo kuwa mlima Kilimanjaro ni watalii kutoka nje ya nchi peke yake, hivyo ipo haja kwa watanzania kuzitembelea hifadhi za taifa zilizopo hapa nchini.

Aidha aliongeza kuwa  Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii, hivyo kuna haja kubwa kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili za nchi zilizpo kwenye hifadhi hizo.

Na Lightness Sebastian, na Leah, walisema ili nchi iweze kupata mapato mengi ipo haja kwa serikali kuendelea kuwahamasisha wanafunzi kuzitembelea hifadhi hasa wanapokuwa likizo ili kuweza kujifunza mazingira zaidi na kuutangaza utalii wa ndani katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa nchi za Afrika.

No comments:

Post a Comment