Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 9, 2014

MWENYEKITI AAMURU WAFUGAJI WOTE WALIOVAMIA MAENEO YA WAKULIMA KUONDOLEWA HARAKA

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya kilosa mheshimiwa Ameir Mubaruk amewaagiza viongozi wa vijiji na kata ya Lumuma iliyopo wilayani Kilosa kuhakikisha katika kipindi hiki cha kiangazi wanawaondoa wafugaji wote wavamizi waliovamia katika maeneo ya wakulima.


Kauli hiyo imetolewa na Mheshimiwa Mubaruk wakati akizungumza na wananchi wa kitongoji  cha Manyomvi kilichopo kata ya lumuma wilayani kilosa katika sherehe ya siku ya mkulima iliyoandaliwa na mradi wa mpango wa kupunguza hewa ukaa inayotokana na uharibifu na ufyekaji ovyo wa misitu MKUHUMI uliopo chini ya shirika la kuifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG.

Mheshimiwa Mubaruk amesema kufuatia kero za wakulima zilizowasilishwa kwake amewaagiza viongozi hao kutekeleza amri hiyo mara moja na pia amesema hakuna ruhusa ya kiongozi wa kijiji kuwapokea wafugaji kiholela bila kufuata taratibu zilizowekwa.

Awali wakitoa kero zao kwa mwenyekiti huyo wananchi hao wameeleza pia kero ya ukosefu wa huduma za kijamii ikiwemo kukosekana kwa barabara,zahanati na shule ambapo wamesema kutokuwepo kwa huduma hizo kunachangia kurudisha nyumba maendeleo ya kitongoji hicho.

Katika hatua nyingine wananchi hao Aidha wamemwomba mwenyekiti huyo kulifikisha ombi la kitongongoji hicho kuwa kijiji  katika baraza la madiwani ili iweze kuwarahisi kupatiwa huduma muhimu ambapo mwenyekiti amelipokea na kuahidi kulifikisha wilayani ili lifanyiwe kazi.

Kwa upande wake afisa kilimo wa mradi wa mkuhumi bwana shadrack yoash nyungwa…..ameelezea lengo la kuadhimisha sherehe hiyo ya siku ya mkulima kuwa ni kupongezana na kupeana zawadi kwa mkulima aliyefanya vizuri shambani kwake sambamba na kupeana zawadi ili iwe chachu kwa wakulima wengine kuongeza juhudi katika kipindi kijacho cha kilimo na kutimiza lengo la mradi la kutoa elimu hiyo.

Vijiji ambavyo vimeshiriki na kupatiwa mafunzo ya kilimo hifadhi na mazingira ni manyomvi,mlenga,idete  na mfuluni, vingine ni kisongwe lunenzi ibingu na chabima.

No comments:

Post a Comment