Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 16, 2014

MIKOA YA KILIMANAJARO, ARUSHA NA MANYARA YAAGIZWA KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

MOSHI serikali ya mkoa wa Kilimanjaro,  Arusha na Manyara, zimeagizwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikiibuka mara kwa mara na kusababisha mapigano baina ya wakulima na wafugaji hao,  hali ambayo imekuwa ikikwamisha shughuli za uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Dkt. Titus Kamani, alipotembelea kituo cha utafiti wa mifugo cha Ranchi ya taifa ya West Kilimanjaro, na kuwataka wakuu wa mikoa hiyo kuzitafutia ufumbuzi migogoro ya mipaka ili maeneo yaliyotengwa yaweze kutumika kama ambavyo yamekusudiwa.

Dkt. Kamani alisema migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ikikwamisha shughuli za uwekezaji katika maeneo mengi, na kwamba hata  uhakika wa usalama wa wawekezaji hao umekuwa wa mashaka kuja kuwekeza hapa nchini.

Waziri kamani, aliongeza kuwa shamba la ranch ya West Kilimanjaro, lilitengwa mahususi kwa  kuzalisha ng’ombe wa nyama ili kuzuia uagizwaji wa nyama kutoka nje ya nchi, jambo ambalo bado halijatimizwa kwa kuwa mpaka sasa bado makampuni ya kitalii na taasisi nyigine yana agiza nyama kutoka nje kutokana na nyama ya hapa nchini kutokidhi vigezo.

Hata hivyo Dkt kamani, aliutaka uongozi wa Ranch hiyo kuhakikisha wanatimiza malengo hayo ili makambuni ya kitalii , migodi na maduka makubwa yaache kuagiza nyama kutoka nje ya nchi na badala yake wanunue nyama hapa nchini ili kuongeza pato la taifa.

Aidha alifafanua kuwa kwa sasa serikali imedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya mifugo kwa kuweka uwekezaji katika uzalishaji wa nyama bora  na ngozi na kuwa hayo hayatawezekana iwapo  wafugaji hawatatoka kwenye ufugaji wa kitamaduni na kuingia kwenye ufugaji wa kisasa.

Kwa upande wake  Meneja wa ranch ya West Kilimanjaro  alisema eneo hilo linaukubwa wa hekta 19,900 zenye uwezo wa kuwa na ng’ombe  6,000 na kwamba kwa sasa ranchi hiyo, ina ng’ombe 170 na kondoo 437.

Akizungumzia changamoto zinazoikabili ranchi hiyo, alisema kuwa ranchi  hiyo inakabiliwa na upungufu wa mifugo ukilinganisha na ukubwa wa eneo, uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa fedha za kuendesha ranchi pamoja na uhaba wa malisho unaosababishwa na wavamizi wa maeneo unaofanywa na wananchi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment