Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 16, 2014

MWENYEKITI NA MTENDAJI WASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE NA UBADHIRIFU

MWENYEKITI wa Kijiji cha Chipanga B, wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Bwana Makasi Kaweya na mtendaji wa kijiji   hicho, wamesimamishwa nyadhifa zao kupisha uchunguzi, kutokana na kutoitisha mikutano ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi kwa zaidi ya miaka mitatu.

Hatua ya viongozi hao kusimamishwa kazi imefikiwa hivi karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Chipanga chini ya mwenyekiti na diwanni wa Kata hiyo bwana, John Daud ambapo kwa kauli moja mkutano huo uliridhia wasimamishwe uongozi.

Tuhuma zinazowakabili ni pamoja na ubadhirifu wa fedha hususani michango ya mfuko wa maji.

Imeelezwa kuwa kero nyingine, ni viongozi  hao kushindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi kwa zaidi ya miaka mitatu.

Baadhi ya wakazi wa kata ya Chipanga wakizungumza na mwanaharakati wa blog hii walisema kuwa kero nyingine, ni udhalilishaji ambapo akina mama wajawazito wanapokwenda kupima afya zao huvuliwa nguo mbele za watu.

No comments:

Post a Comment