Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 16, 2014

MTU MMOJA AFARIKI DUNI NA MWINGINE KUJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI

MWANGA Mtu mmoja mkazi wa Hedaru wilayani same, amefariki dunia papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo, wakati wakifyatua matofali katika eneo la matalang`a wilayani mwanga, mkoa wa Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa kitongoji cha matalang`a, Rasuli H.Mchomvu, alisema aliyefariki dunia ni Kahungo Omary, ambaye mazishi yake yamefanyikia Hedaru wilayani same, huku majeruhi Sila  Sifuni, akiendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Usangi.

Mchomvu alisema, watu hao waliangukiwa na kifusi wakati wakichimba udongo wa kufyatulia matofali pembeni mwa kingo la korongo linalopitisha maji msimu wa mvua lililopo bondeni mahali ambapo kuna asili ya unyevunyevu, julai 14, mwaka huu majira ya saa kumi za jioni.

Alisema walichimba chini ya ukingo wa korongo hilo,ambalo juu yake kulikuwa na matofali hali iliyosababisha ufa katika sehemu hiyo yenye asili ya unyevu na kupelekea kukatika kwa ukingo uliowafukia watu hao,ambapo ulitoa kishindo kikubwa kilichowafikia wenzao waliokuwepo
jirani na eneo hilo.

Hta hivyo mara baada ya watu kufika katika eneo hilo walifanya jitihada za kuwaokoa kwa kutoa kifusi cha udongo kilichowafunika watu hao, ambapo zoezi hilo lilifanikiwa na kumkuta mmmoja akiwa
ameshafariki dunia huku mwenzake akiwa amejeruhiwa vibaya.

Kwa upande wake,Afisa Mamlaka Mkuu wa Mji Mdogo wa mwanga, Ridhiwani Msuya,alikiri kutokea kwa tukio hilo,nakusema kwamba amefariki mtu mmoja huku mwingine akiwa amejeruhiwa;Ambapo aliongeza kuwa polisi walifika kufanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment