KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imempa miezi minne Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Shaaban Ntarambe, awe ametoa maamuzi juu
ya hatima ya wafanyabiashara wa soko la mitumba la Memorial kupatiwa eneo la
soko ambalo litakuwa la kudumu kuliko ilivyo sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama wakati
alipokuwa akiongea na wafanyabiashara wa soko hilo katika mkutano
uliowashirikisha wafanya biashara na wananchi wa kata ya Soweto, ambapo mkuu
mkoa huyo amewataka wafanyabiashara hao kufanya biashara zao kwa uhuru bila ya mtu wa
kuja na kuwabughudhi hadi hapo Manispaa itakapo wapatia eneo la kudumu.
Gama ametoa miezi minne kwa Manispaa wawe wametoa tamko
la hatima ya wafanyabiashara wa soko la Memorial kupatiwa eneo ambalo litakuwa
la kudumu kuliko ilivyo sasa, na kwamba amepiga
marufuku Manispaa kwenda na kuwaondoa wafanyabiashara hao bila ya
kuwapatia eneo ambalo litakuwa la kudumu katika kufanyia biashara zao,.
Ameema wapo watu
wamekuwa wakilichukulia soko hilo kuwa kama medali za siasa katika kuwatishia
wafanyabisahara hao kuwa watakuja kuondolewa na kuwataka wasikubali kuondolewa
hadi hapo Manispaa itakapo wapatia eneo la kufanyia biashara hizo.
Amesema Uchumi wa mkoa wa Kilimanjaro unategemea sana
masoko kama haya, hivyo sitaki kusikia ugomvi unatokea katika soko hili, kuna
watu wachache wamekuwa wakitumia Mamlaka yao kwenda kuwakamata na kuwanyang’anya
bidhaa zao , hili sitaki kulisikia
katika mkoa wangu likijitokeza.
Aidha ameongeza kuwa ni vyema Manispaa wakaharakisha
mchakato wa upatikanaji wa eneo hilo ili wafanyabiashara hao wafanye kazi
ambazo zitakuwa rasmi na kuwepo kwa miundombinu itakayo wezesha upatikanaji wa
huduma zote.
No comments:
Post a Comment