Wakazi wa kata ya Pasua katika manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wanamlalamikia diwani wa kata hiyo Charles Mkarakara kwa kujimilikisha eneo la wazi
lililotengwa kwaajili ya shughuli
maalumu katika kata hiyo.
Malalamiko hayo yametolewa na wakazi hao kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas
Gama, mda mchache baada ya kuweka jiwe la msingi la bweni la wavulana wa shule
ya sekondari ya Anna Mkapa, lililopo katika manispaa ya Moshi mkoani kilimanjaro.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi hao Loti Martin na Dastan Biru walimwambia
mkuu wa mkoa kuwa, wanasikitika kwa kitendo
cha diwani wao kupora eneo ambalo lilitengwa kwajili ya kituo cha mabasi, na badala yake amebadili
matumizi na kujimilikisha eneo hilo na tayari ameanza maandalizi ya ujenzi .
Kufuatia hali hiyo, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonodas Gama
amemwagiza afisa mipango miji wa manispa ya Moshi Alex Poteka na mkuu wa wilaya ya Moshi
Ibrahimu Msengi kusimamisha ujenzi usiendelee katika eneo hilo kisha paitishwe
kikao cha kamati ya maendeleo ya kata (ward c) ili kupata ufafanuzi wa jambo
hilo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Pasua Charles Mkarakara, ambye
pia ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo, amekiri kulifahamu eneo
hilo na kufafanua kuwa eneo hilo ni
mali yake analolimiliki kihalali .
No comments:
Post a Comment