Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 3, 2014

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKEMEA UJENZI M'BOVU WA MAJENGO YA SHULE

KILIMANJARO serikali  mkoani  Kilimanjaro imewataka wahandisi ambao wanasimamia shughuli za majengo wasimamie kwa kufuata sheria,  taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali ili kuondoa uchakachuaji ambao umekuwa ukifanywa na wakandarasi hao.

Kauli hiyo ameitoa jana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, wakati alipotembelea  ujenzi wa bweni la wasichana wa shule ya sekondari Anna Mkapa,  iliyopo katika kata ya Pasua manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, mradi ambao unajengwa kwa fedha za SEDP, ambapo hadi kukamilika kwa ujenzi huo, unatarajiwa kutumia shilingi za kitanzania milioni mia mbili thelathini (230,000,000).

Gama  amesikitishwa na jengo hilo kujengwa chini ya kiwango huku akiwataka  wataalamu waliokagua matofali yaliyotumika kujenga jengo hilo kumpelekea taarifa  kama kweli walifanya ukaguzi huo.


Amesema amesikitishwa kuona kiasi cha saruji kilicho changanywa katika utengenezaji wa matofali yaliyojengea shule hiyo kuwa chini ya kiwango na kumtaka mkandarasi huyo kutoa maelezo ya kina kama kweli matofali hayo yalifanyiwa ukaguzi.


Aidha aliongeza kuwa fedha nyingi za serikali zimekuwa zikipotea kutokana na miradi yake mingi ya ujenzi kujengwa chini ya viwango hali ambayo inalazimu kubomolewa na kuanza kujengwewa upya.

Mara baada ya kusomewa taarifa ya mradi wa  ujenzi huo,  Gama alilazimika kutoa karipio kwa wasimamizi wa jengo hilo kuwa halina ubora, hivyo haliwezi  kunusuru maisha ya wanafunzi hao.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Tilya Construction, Gastor Tilya,  alikiri na kusema kuwa yapo mambo madogo madogo ambayo yanaweza kurekebishwa ingawa alisema yako nje ya uwezo wake.

Naye Mkandarasi ambaye anasimamia ujenzi huo, Frank Msuya amesema kuwa watahakikisha kiwango cha matofali yanayotumika yanakuwa katika ubora unaokubalika.

No comments:

Post a Comment