Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 3, 2014

MSAFARA WA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO WAPOTEZWA

Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ulipotezwa na waongozaji na kupelekwa kwenye eneo ambalo halikuwa limepangwa kwa kile kinachoaminika kuwa ni kuficha ukaguzi wa miradi ya maendeleo mkoani humo.

Leonidas Gama alikuwa katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea kukagua na kufungua miradi ya maendeleo iliyoko ndani ya Manispaa ya Moshi, akiwa ameambatana na wataalamu mabalimbali wa idara wa Manispaa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chanzo chetu imebainisha kuwa msafara ulipofika katika Kata ya Rau ulipotezwa wakati wakienda kukagua upandaji wa miti katika Shule ya Msingi Moshi.

Licha kupotezwa huko, RC Gama alifanikiwa kufika na kukagua miti iliyopandwa ambapo aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuongeza jitihada ya upandaji miti ili kukabiliana na Mabadiliko Tabia Nchi.

Miti 948,220 imepandwa katika Manispaa ya Moshi tangu majira ya mvua yaanze mwaka huu. Msafara wa mkuu wa mkoa ulikuwa ukiongozwa na Mkuu wa Polisi wilaya (OCD) ya Moshi.

No comments:

Post a Comment