Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 3, 2014

MSAADA WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KATIKA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU

MOSHI watoto 21 wenye ulemavu waakili wanaolelewa katika kituo cha faraja home kilichopo katika kijiji cha chekereni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula baada ya mfadhili wa kituo hicho kusitisha huduma, huku akimtaka mmiliki wa kituo kupunguza idadi ya watoto waliopo katika kituo hicho. 

 Huduma hiyo imesitishwa mwaka huu na Mfadhili ambaye ni raia wa Ujerumani kwa madai kuwa kwa sasa uwezo wake ni kuwahudumia watoto 10 kati ya 21 hivyo wahusika hawanabudi kupunguza idadi ya watoto kituoni hapo, hali ambayo imekuwa ni changamoto kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Mmiliki wa kituo hicho Bi. Martha Minja ameyasema hayo baada ya kupokea msaada wa vyakula mbalimbali vikiwamo Sukari, mchele, mafuta na sabuni, vyenye thamani ya shilingi laki sita (600,000), kutoka kanisa la TAG jimbo la Kilimanjaro, ambapo alisema  matatizo yanayowakabili watoto hao ni ukosefu wa matibabu na chakula. 

Voxs pops-Jackline Mushi -mlezi wa watoto wa kituo cha faraja home

Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo makamu askofu wa kanisa la TAG jimbo la Kilimanjaro Mchungaji Redson Ifandi, alisema kanisa hilo limeguswa na changamoto zilizopo kituoni hapo ,na kwamba kanisa la TAG halitachoka kutoa misaada ya hali na mali, pia ameiomba serikali, jamii na taasisi mbalimbali kuwasaidia watu wenye matatizo badala ya kuwategemea wafadhili kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment